Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye maisha huwa kuna kafara ambazo mtu unapaswa kuzitoa ili upate kile unachotaka. Na kadiri kile unachotaka kinavyokuwa kikubwa, ndivyo kafara unayopaswa kutoa inakuwa kubwa.
Kupata maarifa sahihi na usimamizi wa kuyafanyia kazi ni hitaji muhimu sana kwenye safari ya mafanikio. Ni kitu ambacho kinapatikana kwa nadra sana.
Kwa bahati nzuri sana, wewe umeipata fursa ya kupata maarifa sahihi na usimamizi wa kuyafanyia kazi, kupitia Kocha Dr. Makirita Amani.
Katika kuhakikisha watu wengi zaidi wananufaika na maarifa na miongozo anayotoa, huduma nyingi za Kocha Dr. Makirita Amani zimekuwa zinatolewa bure au kwa gharama nafuu zaidi.
Kwa baadhi ya watu wamekuwa wanatumia huduma hizo za bure na kupiga hatua, wakati baadhi wanachukulia kwa mazoea na kutokuthamini.

Ili kuhakikisha nguvu anazoweka zinakuwa na tija, Kocha Dr. Makirita Amani anakwenda kuweka mchujo mkali wa watu anaofanya nao kazi kwa karibu, kwenye kuwapatia maarifa na usimamizi wa mafanikio.
Na mchujo wa kwanza ni ushiriki kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024. Sifa ya kwanza kabisa ya mtu kuweza kupata huduma nyingine za Kocha itakuwa ni ushiriki wa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA.
Hata kama mtu hawezi kumudu mengine, anapaswa kujitoa kafara kwa namna anavyoweza ili kushiriki semina ambayo ndiyo tiketi muhimu kwenye kupata huduma nyingine.
Kocha atakuwa tayari kuwasaidia wale wenye nia ya kufanikiwa hata kama hawawezi kumudu gharama, lakini ni kama tu watakuwa wameshiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA.
Hivyo basi rafiki, fanya kila linalopaswa kufanyika ushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024. Taarifa kamili za semina zipo hapo chini.
Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.
Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.
Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;
1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.
2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.
3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.
4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.
5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.
6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.
7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha
Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.
Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.
Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.
Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.
Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977175 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.
Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi