3557; Wa mwisho ndiye mshindi.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,

Kwa mafanikio yoyote unayoyataka kwenye maisha yako, kuna ushindani mkali utakaokutana nao.

Unaweza kuona njia bora ya kukabiliana na ushindani huo ni kukabiliana nao moja kwa moja.

Lakini kufanya hivyo haiwezi kukusaidia.
Unapokabiliana na ushindi moja kwa moja unaishia kujichosha na kuwa dhaifu, kitu kinachokupeleka kwenye kushindwa.

Njia bora ya kuushinda ushindani ni kuweza kudumu muda mrefu zaidi.
Kwenye ushindani, wa mwisho ndiye mshindi.

Hivyo wajibu wako mkubwa ni kujiuliza ni kwa namna gani unaweza kudumu kwa muda mrefu zaidi ya wengine wowote.

Kwa kila maamuzi unayofanya, swali la kwanza kujiuliza ni kama yatakuwezesha kudumu kwa muda mrefu zaidi kuliko wengine.

Kwa mambo yote unayofanya, jijenge kwa namna ambayo utaweza kudumu kwenye ufanyaji kwa muda mrefu zaidi.

Pale ushindani unapojitokeza, jiambie wazi kwamba hakuna kitakachokuondoa mapema.

Ili hilo liwezekane, ni lazima use na mfumo imara wa kufanya mambo yako ili kupata matokeo bora mara zote.

Unapokuwa umejijengea uimara fulani unaokupa nguvu ya kufanya kwa muda mrefu zaidi, ushindi unakuwa wa uhakika kwako.

Watu wengi hawafanikiwi kwa sababu hawawezi kudumu kwenye kitu kimoja kwa muda mrefu.
Wanahangaika na mambo mengi ambayo yanawadhoofisha na kuishia njiani.

Wewe ukiweza kuwa mtu unayedumu kwenye kitu kwa muda mrefu kuliko watu wengine wote, lazima utapata ushindi.

Rafiki, ni kitu gani umechagua kukifanya kwa muda mrefu na kutoruhusu yeyote kukuondoa?
Hapo ndipo unapoweza kujenga mafanikio yako makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe