Rafiki yangu mpendwa,

Kwa muda sasa tumekuwa tunakupa habari njema za SEMINA YA USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI 2024. Hii ni semina inayokwenda kukujengea ujuzi wa aina tatu; KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha ili kuwa na maisha huru.

Semina hii inafanyika tarehe 27/10/2024 Mbezi Garden Hotel Dar es salaam na ni ya kuhudhuria ana kwa ana.

Kumekuwa na maombi ya watu wengi ambao wanataka sana kushiriki semina hii, ila wanakwama kutokana na umbali na kubanwa na majukumu mengine.

Kwa sababu tunataka kila mtu ayapate mafunzo haya muhimu sana, tumetafuta fursa ya kila mtu kuweza kushiriki akiwa popote.

Hivyo nina habari njema zaidi kwako leo kuhusu kushiriki SEMINA YA USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI 2024 kwa njia ya mtandao.

Kama unataka kushiriki semina lakini uko mbali, tukio zima la semina litarushwa mubashara (live) kwa njia ya video na utaweza kushiriki ukiwa popote.

Na kama utakuwa umebanwa na majukumu wakati wa tukio kutakuwa na rekodi ambayo utaweza kuja kupata masomo yote ya semina kwa njia ya video.

Kupata fursa hii ya kushiriki semina, iwe ni moja kwa moja, kufuatilia kwa mtandao au kupata rekodi, lipa ada ambayo ni Tsh 65,000/= kabla ya tarehe 01/10/2024.

Taarifa zaidi kuhusu semina zipo hapo chini. Karibu sana.

Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.

Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.

Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;

1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.

2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.

3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.

4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.

5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.

6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.

7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha

Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.

Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.

Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024, pia itarushwa live kwa mtandao na kutakuwa na rekodi nzima ya video.

Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.

Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0713604101 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.

Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi