Rafiki yangu mpendwa,
Falsafa yangu kuu kwenye maisha ni; Naweza kupata chochote ninachotaka kama nitawasaidia wengi zaidi kupata kile wanachotaka.
Falsafa hiyo ndiyo imekuwa inaniongoza mara zote kwenye mambo yote ninayofanya. Na ndiyo maana nimekuwa nakazana kukupa wewe thamani kubwa sana kwenye huduma zote ninazotoa.
Nimekuwa sina wasiwasi kwenye kupata yote ninayotaka kwenye maisha yako, kwa sababu najua wajibu wangu ni mmoja tu, kukupa wewe kile unachotaka. Nipo tayari kwa hilo kwa kipindi chote cha maisha yangu.
Lakini kama hata maandiko yanavyosema, Mungu huwasaidia wale wanaoonyesha jitihada za kujisaidia wao wenyewe. Pamoja na uwezo mkubwa ambao Mungu anao wa kumpa mtu chochote anachotaka, ni lazima mtu huyo awe tayari kuchukua hatua fulani ndiyo apate anachotaka.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwa upande wangu, pamoja na utayari wangu wa kukusaidia upate unachotaka, ni lazima wewe mwenyewe uwe tayari kujisaidia mwenyewe. Lazima uwe unataka makubwa na uwe tayari kuyapambania. Lazima ufanye hayo kwa vitendo na siyo maneno tu.

Moja ya vitu ambavyo nakuomba ufanye ili nipate fursa ya kukusaidia kupata unachotaka ni wewe kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 itakayofanyika tarehe 27/10/2024.
Nitaweza kufanya kazi kwa karibu na wale tu watakaoshiriki semina hiyo, kwa sababu kuna miongozo muhimu nitakayoitoa kwenye mafunzo hayo ya semina. Karibu sana ushiriki semina ili tushirikiane kupata unachotaka.
Habari njema ni kwamba unaweza kushiriki semina hii hata kama upo mbali na umebanwa na majukumu mengine. Soma hapo chini kupata taarifa kamili.
Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.
Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.
Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;
1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.
2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.
3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.
4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.
5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.
6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.
7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha
Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.
Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.
Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024, pia itarushwa live kwa mtandao na kutakuwa na rekodi nzima ya video.
Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.
Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0713604101 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.
Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi