Habari njema Matajiri Wawekezaji,
Nichukue nafasi hii kuwapongeza kwa mchakato wa uwekezaji ambao tunaendelea nao kwenye programu yetu ya NGUVU YA BUKU.
Hii ni programu maalumu ya kuwekeza kidogo kidogo, kwa muda mrefu na msimamo bila kuacha. Lengo letu kuu ni kufikia uhuru wa kifedha ili kuwa na maisha huru.
Wakati tunaanza programu hii mwishoni mwa mwaka 2023 na rasmi tarehe 01/01/2024, hatukujua ni kwa ukubwa kiasi gani itapokelewa. Lakini mpaka kufika mwezi Septemba 2024, zaidi ya watu 250 wamepita kwenye programu hii. Japo siyo wote ambao wamekuwa wanawekeza kwa msimamo, lakini watu wote hao wamefungua akaunti na kufanya uwekezaji UTT.
Haya ni mafanikio makubwa ya programu hii, hasa ukizingatia mwamko mdogo ambao watu wengi wanao kwenye uwekezaji. Na tukiweza kuendelea hivi kwa miaka 10 kama ilivyo lengo letu, tutaweza kufikia wengi zaidi na kuleta mapinduzi makubwa.
Huu ni ushindi kwetu sote ambao tunashiriki programu hii, kwa sababu ushiriki wetu na kuwashirikisha wengine kumefanya wengi kujua na kupata msukumo wa kuendelea kuwekeza.

Katika kuendelea kupata elimu, hamasa na mipango bora ya kufanya uwekezaji, tuna semina ya USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI. Semina hii itafanyika tarehe 27/10/2024. Hii ni semina muhimu sana kwetu kushiriki, kwa sababu inagusa eneo hili la fedha na uwekezaji ambalo ndiyo tunalifanyia kazi hapa kwa vitendo.
Lakini pia kushiriki semina hii ni sehemu ya kuwa na mchango kwenye maendeleo ya programu yetu hii ya NGUVU YA BUKU. Kwa sababu kama tunavyojua, programu hii ni bure kabisa kushiriki, japo ina gharama za kuiendesha. Lakini kiu yetu imekuwa ni watu wapate manufaa kwanza na hatimaye watakuwa na michango kwa namna mbalimbali.
Hii ni moja ya fursa kwako mshiriki wa programu ya NGUVU YA BUKU kuwa na mchango wa kurudisha kwenye programu. Na hatukuombi urudishe tu, bali ushiriki mafunzo ambayo yatakufanya wewe kuwa bora zaidi katika utekelezaji wa mipango ya programu hii.
Awali semina hii ilikuwa ya kushiriki kwa kukutana ana kwa ana pekee. Lakini kutokana na umbali wa maeneo ambayo watu wengi wapo, walikuwa wanakwama.
Hilo limetufanya tutafute mfumo wa kuweza kuendesha semina hii kwa washiriki wa ana kwa ana na kwa mtandao kwa ambao wapo mbali. Lakini pia baada ya semina kutakuwa na rekodi ya tukio zima, hivyo hata ambaye hataweza kufuatilia moja kwa moja, ataweza kuyarejea masomo yote kwa rekodi itakayokuwepo.
Mfumo wa kurusha moja kwa moja semina kwa njia ya mtandao pamoja na kuandaa rekodi ya tukio zima una gharama kubwa. Hivyo inahitajika watu wengi zaidi kuweza kushiriki kwa njia hiyo ili iweze kufanyika vizuri.
Hivyo ombi letu kwako mshiriki wa programu ya NGUVU YA BUKU, ambaye ulishindwa kuthibitisha kushiriki semina kwa sababu ya umbali na kukosa muda ni uthibitishe kushiriki kwa njia ya mtandao na kupata rekodi ya mafunzo.
Ada ya kushiriki kwa njia ya mtandao na kupata rekodi ni Tsh 65,000/= kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na baada ya tarehe hiyo ada itakuwa Tsh 100,000/=.
Ni mategemeo yetu kwa kila mshiriki wa programu ya NGUVU YA BUKU kushiriki semina hii ya USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI kwa njia itakayomfaa. Kwa wenye nafasi kushiriki ana kwa ana ni bora zaidi. Kwa watakaokosa nafasi kushiriki live na kupata rekodi itafaa zaidi.
Tutakwenda kuwa na maboresho ya programu yetu ya NGUVU YA BUKU, ikiwepo kuwa na applikesheni maalumu ambayo itatuwezesha kufuatilia vizuri maeneo yote ya fedha, ikiwepo kuongeza kipato, kudhibiti matumizi, kuondoka kwenye madeni na kufanya uwekezaji.
Hayo yote tutajifunza kwenye semina hii ya USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI ili tuzidi kuwa imara kwenye eneo la kifedha.
Kama ulikuwa hujapata taarifa za semina hii, zipo hapo chini kwa ufupi, karibu upitie kisha kuthibitisha ushiriki wako ili tuweze kuendelea na maandalizi mazuri.
Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.
Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.
Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;
1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.
2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.
3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.
4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.
5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.
6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.
7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha
Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.
Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.
Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024, pia itarushwa live kwa mtandao na kutakuwa na rekodi nzima ya video.
Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.
Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0713604101 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.
Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.
MJADALA WA SOMO.
Karibu ushiriki mjadala wa somo hili kwa kushirikisha uliyojifunza na hatua unazokwenda kuchukua kutokana na somo hili.
1. Ni kitu gani kimoja unachojivunia nacho kwa kuwa kwenye programu ya NGUVU YA BUKU?
2. Je umeshathibitisha kushiriki semina na kufanya malipo ya ada? Kama bado shirikisha nini kinachokukwamisha.
3. Ni mtu gani mmoja ambaye ungependa kushiriki naye kwenye hii semina? Je umeshamshawishi aweze kuja? Na kama kuna namna anakwama, unaweza kumsaidia ili ashiriki semina na kujifunza?
4. Kama huna mpango kabisa wa kushiriki semina hii, siyo kwa ana kwa ana, wala live wala rekodi, shirikisha kwa nini umekuwa na maamuzi hayo.
5. Karibu kwa maswali, ufafanuzi na ushuhuda wowote ulionao juu ya somo hili na programu nzima ya NGUVU YA BUKU.
Kila mshiriki wa programu ya NGUVU YA BUKU karibu utume mrejesho wako kwenye somo hili kwa kujibu maswali hayo.
Asanteni na karibuni tuendelee kuwa pamoja kwenye programu yetu ya NGUVU YA BUKU.
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.