3561; Shida huwa zinazidi hapa.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafik yangu mpendwa,
Maisha huwa yana shida na taabu mbalimbali.
Tangu kuzaliwa kwetu ni shida na taabu.
Ukiwa huna unachotaka ni shida.
Na hata ukipata unachotaka ni shida.
Pamoja na hizo shida ambazo tumeshazizoea, huwa kuna wakati ambapo shida huzidi kuliko kawaida.
Wakati huo ni pale unapokuwa unakaribia kufikia makubwa ambayo umeyapambania sana.
Hapo ndipo utapigwa vita ya kila aina, kuanzia ndani yako mpaka nje yako.
Vikwazo vya kila aina vitaibuka kukuangusha usifikie kilele ambacho unakikaribia.
Huo ndiyo wakati ambao wengi hukata tamaa na kuacha kufanya na kuwa wamepoteza kabisa kile walichojenga kwa muda mrefu.
Rafiki, ninachotaka utoke hapa ni kitu kimoja, pale mambo yanapokuwa magumu kuliko ulivyozoea, jua kuna makubwa ambayo unayakaribia.
Endelea kukaza hapo hapo, usilegeze kamwe, kwani ukivumilia kidogo tu, unakwenda kubadili kila kitu.
Ni mara ngapi umekata tamaa na kuacha kufanya kitu na baadaye kuja kugundua ulikuwa karibu sana na ndoto zako wakati unaacha?
Usikubali hilo lijirudie tena, ukishakata shauri kwamba unataka kitu, kipambanie mpaka ukipate, hakuna kuishia njiani.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe