Rafiki yangu mpendwa,

Kwa muda sasa tumekuwa tunakupa habari njema za SEMINA YA USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI 2024. Hii ni semina inayokwenda kukujengea ujuzi wa aina tatu; KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha ili kuwa na maisha huru.

Semina hii inafanyika tarehe 27/10/2024 Mbezi Garden Hotel Dar es salaam na ni ya kuhudhuria ana kwa ana.

Ili kufanya maandalizi bora ya semina hii, kila mshiriki aweze kupata mafunzo bora na kubadili maisha yake, uthibitisho unapaswa kuwa mapema.

Na leo tarehe 30/09/2024 ndiyo siku ya mwisho kwako kulipia ili uweze kupata nafasi ya kushiriki semina ya USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI kwa gharama nafuu.

Kuanzia kesho tarehe 01/10/2024 gharama za kushiriki semina zitapanda kutoka Tsh 65,000/= mpaka kufika Tsh 100,000/=.

Semina hii inafanyika kwa njia ya kukutana ana kwa ana, kwa njia ya mtandao na pia kuweza kupata rekodi ya mafunzo yote. Hivyo unaweza kushiriki ukiwa popote na hata kama muda umekubana.

Rafiki, umeshasikia sana kuhusu semina hii na tayari una maamuzi kama ni kitu kinachokufaa au la. Wito wangu kwako ni ufanye malipo leo, usiendelee tena kusubiri.

Kitu kimoja ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba malipo utakayofanya leo ni uwekezaji bora kabia utakaokuwa umeufanya kwenye maisha yako.

Taarifa zaidi kuhusu semina zipo hapo chini. Karibu sana.

Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.

Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.

Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;

1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.

2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.

3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.

4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.

5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.

6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.

7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha

Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.

Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.

Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024, pia itarushwa live kwa mtandao na kutakuwa na rekodi nzima ya video.

Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.

Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0713604101 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.

Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi