3577; Kama hulipwi, usifanye.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,

Maisha tayari ni magumu, ila huwa tunazidi kuongeza ugumu wake kwa kufanya mambo ambayo siyo tu hayana manufaa, bali yanatuongezea matatizo.

Moja ya mambo hayo tunayopenda sana kufanya na yanakuwa matatizo kwetu ni kuwasahihisha watu ambao wanakosea.

Huwa tunapata msukumo wa kuwasahihisha watu ambao tunaona wanakosea.
Lakini hilo huwa haliishi vizuri, kwani huibua changamoto ambazo zinatusumbua zaidi.

Wale tunaojitolea kuwasahihisha, huwa wanaishia kutuchukia na hapo mambo kuwa magumu zaidi.

Kinachofanya kuwasahihisha tunaoona wanakosea kuwa changamoto ni;

Moja; wenyewe kuwa wanajua wanakosea, ila wanafanya kwa makusudi fulani.

Mbili; wenyewe kuona wako sahihi na wanaowakosoa ndiyo wanakosea.

Tatu; wenyewe kuwa sahihi na wanaokosoa ndiyo wanaokosea.

Kwa vyovyote vile, kumsahihisha anayekosea huwa haiishi salama.

Labda kama mtu huyo amekuomba, tena kwa kukulipa umsahihishe anapokosea.

Ndiyo kusema kama hulipwi kwa kuwasahihisha wanaokosea, usifanye hilo.

Peleka hizo rasilimali kwenye kufanya mambo ambayo yanakulipa zaidi.

Utayafanya maisha yako kuwa bora na kuondokana na changamoto nyingi kwa utaacha kuwasahihisha wale wanaokosea kama hawakulipi kufanya hivyo.

Rafiki, ni mara ngapi umewasahihisha watu kwa nia njema kabisa lakini wakaishia kukuchukia na mambo yakaharibika zaidi?
Umeshajifunza hilo kwa njia ngumu, usitudie tena kosa. Wasahihishe watu kama unalipwa kwa kufanya hivyo.
Tofauti na hapo, pambana kufanya yako.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe