HUDUMA ZA UKOCHA 2024 – 2025.

Rafiki yangu mpendwa,

Karibu kwenye huduma za ukocha kwa mwaka wa mafanikio 2024 – 2025.

Msingi mkuu wa huduma hizi ni MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO.

Kupitia huduma hizi unayapata MAARIFA sahihi kupitia MAFUNZO na USHAURI utakaokuwa unapewa. Pia utapata USIMAMIZI wa kuyaweka maarifa kwenye VITENDO na hilo kukuwezesha kupata mafanikio.

Kwa mwaka huu wa mafanikio 2024 – 2025 kuna huduma kuu nne za ukocha.

HUDUMA YA KWANZA; UTAJIRI.

Hii ni huduma ya ukocha inayokuwezesha kujijengea NGUZO SABA za USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI.

Kwa kuwa kwenye huduma hii utaweza kupata matokeo yafuatayo;

1. Kukuza kipato chako.

2. Kudhibiti matumizi yako.

3. Kuweka akiba.

4. Kuondoka kwenye madeni.

5. Kufanya matoleo.

6. kufanya uwekezaji.

7. Kuwa na ulinzi (bima).

8. Matumizi ya UTAJIRI.TZ app kwa usimamizi wa fedha.

Kwenye huduma hii unapata vipindi vya mafunzo vya kila siku, unapata ushauri kwenye nguzo hizo saba na kusimamiwa kwenye utekelezaji.

Ada ya huduma hii ni Tsh 1,000,000/= (Milioni Moja) kwa mwaka, ambayo unaweza kuilipa kwa awamu moja, mbili au nne.

HUDUMA YA PILI; MAUZO.

Hii ni huduma ya ukocha inayokuwezesha KUKUZA MAUZO kwenye biashara yako.

Kwa kuwa kwenye huduma hii utaweza kupata matokeo yafuatayo;

1. Kuwa na mfumo mzuri wa mauzo kwenye biashara yako.

2. Kujenga timu bora ya mauzo.

3. Kuongeza wateja wapya kwenye biashara.

4. Kukuza mauzo ya biashara.

5. Kuwabakiza wateja kwa muda mrefu kwenye biashara.

6. Kuiona fedha ya biashara kwa kuwa na mzunguko chanya wa fedha.

7. Matumizi ya CHUO CHA MAUZO app kwa mafunzo ya MAUZO.

Kwenye huduma hii unapata huduma ya UTAJIRI na manufaa yake pia. Pia unapata vipindi vya mafunzo vya kila wiki, unapata ushauri kwenye mauzo na kusimamiwa kwenye utekelezaji.

Ada ya huduma hii ni Tsh 3,000,000/= (Milioni Tatu) kwa mwaka, ambayo unaweza kuilipa kwa awamu moja, mbili au nne.

HUDUMA YA TATU; BILIONEA.

Hii ni huduma ya ukocha inayokuwezesha KUJENGA MFUMO wa kuendesha biashara yako.

Kwa kuwa kwenye huduma hii utaweza kupata matokeo yafuatayo;

1. Kuwa na mfumo mzuri wa kuiendesha biashara yako.

2. Kujenga timu bora ya kuendesha biashara.

3. Biashara kuweza kujiendesha bila kukutegemea moja kwa moja

4. Kupata usimamizi wa biashara kutoka kwenye bodi ya wakurugenzi.

5. Kupata fursa za kukuza mtaji wa biashara.

6. Kuongeza ufanisi na kukuza faida ya biashara.

7. Matumizi ya MAUZO.TZ CRM & ACCOUNTING kwa usimamizi wa biashara.

Kwenye huduma hii unapata huduma ya UTAJIRI na MAUZO na manufaa yake pia. Pia unapata vipindi vya usimamizi wa biashara vya kila wiki, unapata ushauri kwenye kukuza biashara na kusimamiwa kwenye utekelezaji.

Ada ya huduma hii ni Tsh 10,000,000/= (Milioni kumi) kwa mwaka, ambayo unaweza kuilipa kwa awamu moja, mbili au nne.

HUDUMA YA KWANZA; BINAFSI.

Hii ni huduma ya ukocha inayokuwezesha KUTEKELEZA MALENGO NA MIPANGO makubwa ambayo mtu unakuwa nayo.

Kwa kuwa kwenye huduma hii utaweza kupata matokeo yafuatayo;

1. Kuwa na MATAMANIO makubwa ya kufanikiwa kwenye maisha.

2. Kuweka MALENGO makubwa na mpango wa kuyafikia.

3. Kujitoa na kuwa na MSIMAMO kwenye kuyafanyia kazi malengo.

4. Kuwa na NIDHAMU kali kwenye kuyafanyia kazi malengo mpaka kuyafikia.

5. Kupata huduma ya ukocha kwa jinsi unavyotaka wewe.

6. Huduma kuwa binafsi kwako na kutolazimika kuwa kwenye kundi na watu wengine.

Kwenye huduma hii unapata nafasi ya kuchagua huduma nyingine yoyote ya ukocha inayotolewa. Pia unapata nafasi kubwa ya kupata ushauri na kusimamiwa kwenye utekelezaji.

Ada ya huduma hii ni Tsh 20,000,000/= (Milioni Ishirini) kwa mwaka, ambayo unaweza kuilipa kwa awamu moja, mbili au nne.

VIPINDI VYA MAFUNZO, USHAURI NA USIMAMIZI.

Ratiba za vipindi vya mafunzo, ushauri na usimamizi kwenye huduma hizi inakuwa kama ifuatavyo.

1. Kila siku, jumatatu mpaka jumamosi kunakuwa na vipindi vya mafunzo vya ONGEA NA KOCHA, saa 11 alfajiri mpaka saa 12. Vipindi hivi ni mubashara (live) na wote walio kwenye huduma wanapaswa kushiriki (Isipokuwa kwa huduma binafsi ambapo mtu anachagua).

2. Kila jumamosi kuanzia saa 12 mpaka saa 2 asubuhi kunakuwa na kipindi cha mafunzo cha CHUO CHA MAUZO ambapo timu yako ya mauzo inashiriki. Kipindi hiki ni kwa walio kwenye huduma ya MAUZO kwenda juu.

3. Kila jumapili kuanzia saa 11 mpaka 1 asubuhi kunakuwa na kipindi cha BILIONEA MAFUNZONI ambacho ni cha usimamizi wa biashara. Kipindi hiki ni kwa walio kwenye huduma ya BILIONEA kwenda juu.

4. Kila kwezi kunakuwa na mkutano wa tathmini ya biashara ambao unafanyika kwa njia ya mtandao.

5. Kila robo mwaka kunakuwa na mkutano wa kukutana ana kwa ana wa kupata tathmini ya maendeleo ya biashara kulingana na malengo ya mwaka yaliyowekwa.

6. Kunakuwa na mazungumzo ya kila mshiriki na Kocha; kila mwezi kwenye huduma ya UTAJIRI, kila wiki kwa MAUZO na BILIONEA na kila siku na inapohitajika kwa BINAFSI.

7. Kuwa kwenye huduma yoyote ya ukocha unakuwa kwenye BILIONEA MAFUNZONI CLUB ambayo ni klabu ya USIMAMIZI na UWEKEZAJI wa biashara zilizopo ndani ya huduma.

Rafiki, kama kweli umedhamiria kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako, hakuna mahali pengine unapopaswa kuwa bali kwenye huduma hizi za UKOCHA. Anza na huduma unayoweza kuimudu na kuifanyia kazi kisha tumia mafunzo, ushauri na miongozo unayopata kukua zaidi.

Kupata huduma ya ukocha unapaswa kujaza fomu kwa kuweka taarifa zako, kuchagua huduma utakayoanza nayo na kuweka malengo yako.

Fomu ya kujaza inapatikana kwa KUBONYEZA MAANDISHI HAYA. Au fungua link hii moja kwa moja; https://forms.gle/KbzyT1FKycMWSTnX9

Kwa maelezo zaidi wasiliana na namba 0717101505.

Karibu sana rafiki yangu tufanye kazi kwa karibu kwa mafanikio yako makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

www.mafunzo.mauzo.tz