3595; Akili za bure.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Akili huwa inaonekana ni kitu ambacho mtu anazaliwa nacho.
Yaani ni unazaliwa una akili nyingi au za kawaida.
Kujifunza huwa ni sehemu ya kuchochea akili, lakini huwa haionyeshi kubadili hali ya akili ya mtu.
Hilo hupelekea wengi kuamini akili walizozaliwa nazo ndiyo hizo hizo wanaweza kuwa nazo.
Lakini hiyo siyo kweli, upo uwezo wa watu kuongeza akili zao na ikawa na manufaa makubwa kwao.
Njia ya kufanya hivyo ni kuwa na shauku kubwa.
Kuwa na shauku inaongeza alama za akili kwa mtu.
Hiyo ni kwa sababu shauku inampa mtu msukumo wa kufanya makubwa.
Pia shauku huwa inawafanya watu kuwa na ushawishi mkubwa kwa wengine.
Kuwa na shauku kunawafanya watu kujiamini wao wenyewe na hata kuaminika na wengine.
Uzuri ni kwamba shauku ni kitu ambacho mtu unaweza kujijengea.
Mtu unaweza kuongeza shauku yako kwa kuigiza kuwa na shauku.
Rafiki, ni mara ngapi umekosa vitu ulivyokuwa unataka kwa kukosa shauku?
Amua sasa kwamba itakuwa ni dhambi kubwa sana kwako kutokuwa na shauku kwenye jambo lolote lile.
Mara zote igiza kuwa na shauku kubwa mpaka iwe sehemu ya maisha yako.
Ukiweza kuwa na shauku kubwa mara zote, itakurahisishia kupata mengi unayotaka.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe