Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye safari yako ya kujenga utajiri, ni lazima mara zote urudi kwenye msingi kwamba SIRI KUU YA KUJENGA UTAJIRI NI KUWA BAHILI.
Najua kusikia tu UBAHILI tayari umejisikia vibaya, kwa kuona ni kujitesa.
Lakini UBAHILI siyo kujitesa, bali kuwa na matumizi madogo kuliko kipato chako.
Kwa bahati mbaya sana, mara kwa mara umekuwa na matumizi makubwa kuliko kipato chako.
Na hapo ndipo shida zako nyingi za kifedha zinapoanzia.
Kwenye kitabu cha NGUVU YA BUKU, nimekushirikisha njia 300 za kuweza kutoka kwenye shimo hilo la matumizi kuzidi kipato.
Na moja ya njia hizo ni ile ya 22 ambayo inasema; Kunywa Maji Badala Ya Vinywaji Vingine.

Kuna vinywaji vingi huwa unakunywa na ambavyo vina gharama.
Lakini vinywaji hivyo havina manufaa yoyote ya ziada kwenye mwili wako.
Mifano ni pombe, soda, juisi na vingine, vyote hivyo havina manufaa.
Tena zaidi vina athari kwako kiafya.
Hivyo moja ya hatua muhimu kwako kuchukua ili kupunguza gharama na kulinda afya ni kufanya maji kuwa kinywaji kikuu kwako.
Kunywa maji peke yake na achana na vinywaji vingine vyote.
Utaokoa fedha nyingi na kulinda afya yako.
Halafu hizo fedha unazookoa sasa, unaziwekeza kupitia programu ya NGUVU YA BUKU.
Rafiki, je umeshaingia kwenye programu hiyo ya NGUVU YA BUKU?
Kama bado, tuma sasa ujumbe wenye maneno NATAKA NGUVU YA BUKU kwenda namba 0678977007.
Karibu sana rafiki yangu tuambatane pamoja kwenye hii safari ya kujijengea utajiri na uhuru wa kifedha.
Rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.