
Rafiki Yangu,
Kuna siri moja ambayo wengi hawaijui mafanikio makubwa hayaanzi na mtaji, wala bahati.
Yanaanzia kichwani.
Ndiyo,
kila kitu kikubwa unachokiona leo majengo, biashara, ubunifu, hata utajiri kilianza kama wazo kwenye akili ya mtu.
Lakini tatizo kubwa ni hili: wengi wanataka mafanikio mapya wakiwa na fikra za zamani.
Wanataka maisha mapya bila kubadilisha namna wanavyofikiri.
Wanataka matokeo makubwa huku bado wanafikiria kama waathirika, si washindi.
Ukweli ni kwamba fikra zako ndizo zinazoamua kiwango cha mafanikio yako.
Kama unaamini huwezi, akili yako itatafuta kila ushahidi wa kuthibitisha hilo.
Utaona vizuizi kila mahali.
Lakini ukibadilisha mtazamo wako, ukianza kuamini inawezekana, akili yako nayo itaanza kutafuta namna ya kufanikisha hilo.
Tatizo la wengi si umaskini, si kukosa elimu, si hata kukosa nafasi.
Tatizo ni mtazamo finyu.
Watu wanakaa wakilalamika, wakisubiri hali ibadilike, wakati ukweli ni kwamba hali hubadilika pale mtu anapobadilika.
Unapobadilisha fikra zako dunia yako yote hubadilika.
Ni kama kubadilisha miwani uliyoivaa; ghafla unaanza kuona vitu kwa uwazi.
Fikiria hili kwa sekunde chache…Ni mara ngapi umekuwa na wazo kubwa, lakini ukajizuia kwa sababu ulihisi hauko tayari?
Ni mara ngapi umeahirisha kuchukua hatua kwa sababu uliona *sasa si muda sahihi*?.
Kila siku unachelewesha mafanikio yako kwa sababu ya woga, mashaka, na maamuzi yanayocheleweshwa.
Hiyo ndiyo nguvu ya fikra hasi inakuibia ndoto zako taratibu bila hata kugundua.
Watu wengi wamefundishwa kuamini mafanikio ni ya wachache tu.
Kwamba kuna *waliobarikiwa* na *wasio barikiwa.*
Lakini hiyo si kweli.
Hakuna mtu aliyezaliwa akiwa na akili ya pesa, wala akili ya mafanikio.
Wote tunazaliwa na akili tupu, tunajifunza kupitia mazingira.
Kama ulilelewa kwenye mazingira ya *haiwezekani,* lazima uanze kujifunza upya.
Huwezi kuishi maisha makubwa ukiwa na imani ndogo.
Ukiendelea kuamini mafanikio ni magumu, utayafanya yawe magumu kweli.
Suluhisho ni moja anza kubadilisha namna unavyofikiri.
Jifunze kuiona changamoto kama fursa.
Amini kwamba unaweza kufanikiwa hata bila mtu kukuamini.
Weka akilini kwamba kila mafanikio makubwa ni matokeo ya uvumilivu, maamuzi sahihi, na mawazo chanya yanayoendelea kuishi hata wakati mambo hayaendi sawa.
Anza kujenga imani mpya kichwani mwako:
Amini kwamba mafanikio ni haki yako.
Amini kwamba unaweza kujifunza chochote.
Amini kwamba unaweza kutoka ulipo sasa, bila kisingizio chochote.
Ukishajifunza kufikiri vizuri, akili yako huanza kukutengenezea njia mpya.
Unaanza kuvutiwa na mawazo mazuri, watu chanya, na fursa zinazokua ambazo zilikuwa mbele yako muda wote,
… lakini hukuziona kwa sababu fikra zako zilikuwa zimefungwa.
Namkumbuka kijana mmoja niliwahi kumfundisha kanuni hii.
Alikuwa amechoka, biashara haikuwa ikienda, kila siku alikuwa analalamika kuwa *hali ni ngumu.
*Siku moja nikamwambia *tatizo si biashara yako, ni kichwa chako.*
Akanitazama kwa mshangao.
Nikamwambia, *anza kuamini biashara yako inaweza kufanikiwa. Jifunze kila siku, fanya maamuzi kwa ujasiri*
Alichukulia kwa uzito.Baada ya miezi sita, akanipigia simu. Akanambia, *Mwalimu, sijui ulitumia dawa gani, lakini mambo yamebadilika.
Nilianza kuamini tofauti, sasa biashara inafanya vizuri.*
Nikatabasamu.
Kwani hakuwa ametumia miujiza, hakuwa amepata mtaji mpya alibadilisha fikra zake.Akili yake ikaanza kuvutia kile alichokuwa akiamini.
Kama unaota mafanikio, tambua hiliNdoto yako haiwezi kukua zaidi ya kiwango cha fikra zako…Fikra zako ndizo zinazoamua wapi utaishia.
Woga, mashaka, na kutojiamini ni vizuizi vikubwa kuliko ukosefu wa fedha.
Badilisha mawazo yako, utaanza kuona dunia kwa jicho jipya.
Wacha hofu ichukuliwe na ujasiri.
Wacha mashaka yamezwei na imani.
Mafanikio hayatokei ghafla yanajengwa ndani yako kwanza, ndipo yanaonekana nje yako.
Kwa hiyo, kabla hujaanza safari ya mafanikio, kwanza jenga akili sahihi ya mafanikio.
Anyway, kama bado hujasoma kitabu kipya cha FALSAFA YA MAISHA YA MAFANIKIO.
Kisome kwani kitafungua macho yako, kitakufundisha kufikiri kama mshindi,na kukupa zana sahihi za kuibadilisha akili yako kuwa chanzo cha mafanikio makubwa.
Hiki Hapa 👇 *https://wa.link/eqqp80*
Karibu.0756694090.
PS: Kabla ya kubadilisha maisha yako, badilisha namna unavyofikiri.Hapo ndipo safari ya mafanikio inaanzia.