Uwezo wa binadamu wa kufikiria hauna mwisho, Ila kwa bahati mbaya tafiti zinaonyesha kwamba asilimia kubwa ya binadamu tunatumia chini ya asilimia tano ya uwezo wa kufikiri. Hata wanasayansi maarufu kama Newton na Einstern inasemekana walitumia chini ya asilimia kumi ya uwezo wa binadamu wa kufikiri.

  Nimeuliza hilo swali kwa makusudi sio kwa sababu hufikirii ila inawezekana hufikirii yaliyo ya msingi zaidi. Kila mtu kwa wakati wowote kuna jambo fulani atakuwa analifikiria na asilimia kubwa ya mawazo ya binadamu imetawaliwa na hofu. unaweza kuwa na mawazo mengi sana ila ukiangalia kwa makini utagundua huenda mawazo yote uliyo nayo yanatokana na hofu ama matatizo. Inaweza kuwa hofu ya ugumu wa maisha, hofu ya kufeli jambo fulani, hofu ya kukataliwa na kadhalika.

  Tunatumia muda mwingi sana kufikiria hizo hofu badala ya kutumia muda huo kufikiri jinsi ya kufikia malengo yako. Ndio maana nimekuuliza mara yako ya mwisho kufikiria ni lini, nikimaanisha kutokufikiria hofu yoyote na kuelekeza akili yako kufikiria njia bora za kufikia malengo yako. Fikiri hivi; kama utafanikiwa kufikia malengo yako uliyojiwekea kwenye maisha(kama umeweka malengo) je utakuwa na hofu yoyote? Kama jibu ni hapana kwa nini basi upoteze muda kufikiria hofu badala ya kuutumia vyema kufikiria njia za kuyafikia malengo yako ambayo yatakuondolea hofu?

  Chanzo kikuu cha hofu ni matatizo yaliyokwisha tokea ama unayohisi yanaweza kutokea. Hofu nyingi sio za kweli, ni za kufikirika tu, hivyo hata ukihofu vipi bado hofu haitkusaidia kuondoa tatizo. Usipoteze muda wako kufikiria matatizo, badala yake utumie vyema kufikiria jinsi ya kufikia malengo yako na kutatua matatizo yako. watu walifanikiwa sio kwamba hawana matatizo ila wamefanikiwa kuyatatua matatizo yao na kuepuka hofu.

  Kuanzia sasa unapofikiri fikiri hasa jinsi ya kutatua matatizo yanayokukabili na jinsi ya kuyafikia malengo yako. usipoteze muda wako kuhofu, hofu haitokusaidia lolote zaidi ya kukuongezea msongo wa mawazo na kufanya maisha yaonekane magumu kuliko yalivyo.