Umewahi kuona shamba lenye rutuba na linalopata mvua za kutosha ila halijalimwa chochote? Je linakuwa tupu bila ya chochote? Jibu nI hapana, litaota magugu na majani mengine mengi yasiyo na faida kwa mwenye shamba. Kwa upande mwingine shamba kama hilo lenye rutuba na linalopata mvua za kutosha likipandwa mazao na kupaliliwa vizuri litatoa mavuno mazuri ambayo yatamnufaisha sana mwenye shamba.
Kila mtu analo hilo shamba ninalolizungumzia, na shamba hilo ni akili yako. Akili yako ni sawa na shamba lenye rutuba na linalopata mvua za kutosha, ila upandaji na upaliliaji wa mazao inategemea na wewe mwenyewe. Utofauti uliopo baina ya binadamu ama kwa waliofanikiwa na walioshindwa ni jinsi ya kulitumia shamba hili. Kwa kuwa shamba hili ni lako wewe binafsi, unaamua mwenyewe matumizi gani unataka, unaweza kulitumia kwa matumizi ya aina tatu;
Unaweza kuamua kupanda mazao mazuri na kupalilia ili upate mavuno mazuri. Hapa ni pale unapoingiza mawazo mazuri kwenye akili yako kila siku, na kuondoa mawazo yote mabaya unayoyapata kila siku. Mawazo haya ni yale yanayokufikisha kwenye malengo yako na unaweza kuyapata kutoka kwa watu, vyombo vya habari, mitandao(kama unavyopata hapa) na kwa kujisomea. Hakuna anaeshindwa kupata mawazo mazuri, ni kuamua tu na kuwa na malengo.
Unaweza kulitelekeza shamba lako kwa kutolilima kabisa, na hapa ndipo asilimia kubwa ya watu tupo. Shamba lililotelekezwa huota magugu na vichaka visivyo na faida kwa mwenye shamba. Hivyo pia kwa akili yako, kama hakuna kitu cha maana unachoingiza basi jua vitaingia vingi visivyo na maana. Kama huna malengo na mawazo mazuri ya kuyafikia malengo yako basi utajikuta unafanya chochote kinachokuja mbele yako. Ni vigumu sana kufanikiwa kama huna mpango wowote kwenye maisha yako.
Pia unaweza kupanda mbegu mbaya kwenye shamba lako, na kuvuna mazao mabaya. Usemi wa UTAVUNA ULICHOPANDA uko sahihi, huwezi kupanda mchicha ukavuna mahindi. Kama mawazo unayoingiza kwenye akili yako ni mabaya au hasi na mavuno yatakuwa ya aina hiyo hiyo.
Amua sasa kumiliki shamba lako, kulilima vizuri, kupanda mbegu njema, kupalilia vizuri na hatimaye kufurahia mavuno mazuri. Shamba tayari unalo lenye rutuba ya kutosha na linalopata mvua za kutosha, ni wewe tu kuchukua hatua. Chukua hatua sasa kutumia rasilimali kuu uliyonayo ambayo ni AKILI YAKO.