Katika jambo moja ambalo watanzania tumebobea ni kukosoa na kukatisha tamaa. Mtu anaweza kuwa na ndoto kubwa ia anapowaambia watu badala ya watu kumsaidia ni jinsi gani anaweza kuifikia ndoto yake wanaanza kumkatisha tamaa kwamba hiyo ndoto haiwezekani.
Hivi karibuni kumekuwa na mvutano kati ya wasanii wawili, ambao ni Sintah na Shilole. Mvutano huo ulianza baada ya shilole kusema atatoa wimbo na Jenifer Lopez msanii wa marekani. Sinta alimpinga Shilole na kusema kwamba HAIWEZEKANI kwa sasa shilole aweze kufanya ushirikiano na msanii huyo mkubwa.
Yawezekana ni kweli kwa sasa ni vigumu kwa shilole kufanya ushirikiano huo, ila sio sahihi kumwambia HAWEZI. Hakuna neno baya kama kuambiwa HUWEZI, inakatisha sana tamaa na kumjengea mtu kutokujiamini.
Kama mtu yeyote anakueleza ndoto yake hata iwe kubwa kiasi gani KAMWE usimwambia huwezi. Badala ya kutumia nguvu nyingi kumweleza ni kwa nini anachowaza hawezi kutekeleza hebu tumia nguvu hiyo kumsaidia ni vipi anaweza kufikia ndoto yake hiyo.
Kumwambia mtu hawezi kufikia ndoto yake, hata kama umemwambia hawezi kwa sasa, tayari umeshamuwekea kikwazo kikubwa.
Uwezo wa akili ya binadamu hauna kikomo, na mtu anaweza kuumba kile anachoota. Kama kweli mtu amedhamiria kufanya kitu na akaweka nguvu zake kwenye kitu hicho lazima atafanikiwa kukifanya.
Kinachowazuia watu wengi kuwa na ndoto ni ukatishwaji tamaa na wanaowazunguka. Unaweza ukawa unaongea tu kwa sababu ni maoni yako lakini madhara ya unachoongea ni makubwa sana kwa mwenye ndoto na jamii kwa ujumla.
Hata siku moja usiudharau uwezo wa binadamu, na usimwambie mtu HAWEZI, lolote inawezekana kama mtu anaamua kufanya kwa nguvu na maarifa yake yote.
oh
LikeLike