Televisheni ni chombo kizuri sana cha habari ambacho kinatupa nafasi ya kuona matukio mbalimbali yanayotokea duniani. Pia televisheni zina vipindi mbalimbai vya kufundisha na kuburudisha.

  Kuna michezo na tamthilia mbali mbali zinazooneshwa kupitia televisheni ambazo zinafundisha, zinasisimua na pia zinaburudisha.

  Pamoja na mazuri hayo ya televisheni kuna watu wanateseka sana na televisheni ama movie. Kuna watu wameshakuwa wateja wa tamthilia ama movies kiasi kwamba wanahisi wasipoangalia watapata ugonjwa.

 tvaddict

Uteja wa tamthilia na movie kama ulivyo uteja ama ulevi mwingine ni kitu kinachoanza taratibu na kukua mpaka kufikia hatua ya kutawala maisha yako. Na kinachoongeza uteja huu ni mbinu mbalimbali za tamthilia za siku hizi. Kuna hizi movies zinazotolewa kwa mfumo wa series na episodes. Kila unapangalia kipande(episode) kimoja, kinakupa hamu ya kujua nini kiiendelea hivyo unaangalia kingine na kingine na kingine unapokuja kustuka umeshaangalia kama episode 10 na unajikuta umeshapoteza zaidi ya saa tatu.

tvaddict2tvaddict3

  Katika vitu ambavyo vinapoteza sana muda wa watu na hasa vijana ni hizi movies na tamthilia. Kama na wewe umeshakuwa mteja wa tv au movie ni vyema ukafanya maamuzi ya kubadili tabia hiyo ili kuweza kuokoa muda unaoupoteza.

  Zipo njia nyingi unazoweza kutumia kuondokana na uteja huu. Hizi hapa ni njia kuu tatu unazoweza kutumia na ukandokana na uteja huo mara moja.

  Kwanza ijue thamani ya muda wako na ujue kila muda unaopoteza kuangalia tv au muvi unapoteza fedha.(soma; thamani ya muda wako). Hakikisha muda unaotumia kuangalia tv ama movie ni muda wako wa mapumziko na usiwe muda mwingi sana. Na pia hakikisha kuna unachojifunza kwenye kile unachoangalia. Ili kuokoa muda unaopoteza kwenye tv fanya kitu kingine kwenye huo muda(soma; jinsi ya kubadili tabia)

  Chagua vipindi vya tv utakavyokuwa unaangalia na pia chagua baadhi ya muvi ama tamthilia utakazotizama. Jua kwamba huwezi kuangalia kila kipindi ama kila movie inayotoka. Kila siku zinatoka movie nyingi mpya na pia kuna vipindi vingi sana vya tv. Ukitaka kutopitwa na chochote utapoteza muda wako mwingi kuangalia tv na movie.

  Njia ya tatu ambayo ni ya muhimu sana kuifikiria kila unapoangaia movie ama tv ni kwamba wale unaowaangalia wanatengeneza pesa, je wewe unatengeneza pesa kwa kuwaangalia? Wae unaowaangalia wanafurahia maisha yao na kuishi ndoto zao, je wewe unafurahia maisha yako na kuishi ndoto zako kwa kutumia muda mwingi kuangalia movie ama tv? Ukipata majibu ya maswali hayo chukua hatua mara moja.