Karibu kwenye utaratibu wa kujisomea vitabu
Kitabu tutakachosoma mwezi huu wa nane ni How to Win Friends and Influence People by Dale Carnegie
Kitabu hiki kinafundisha mbinu mbalimbali za kutengeneza marafiki na kuongeza ushawishi wako kwa watu.
Ni muhimu sana ukakisoma kitabu hiki kwa sababu kwa chochote unachofanya ni muhimu kuweza kuwashawishi watu.
Kama wewe ni kiongozi utaongeza ushawishi wako kwa watu na hivyo mawazo yako kukubalika.
Kama wewe ni mwajiriwa utapata mbinu za kuweza kufanya kazi vizuri na wenzako na pia kuweza kumshawishi bosi wako kwa wazo lolote ulilonalo.
Kama wewe ni mfanya biashara usiache kukisoma kitabu hiki kwa sababu utapata mbinu zitakazokusaidia kuongeza wateja na kupata faida kubwa.
Hata kama haupo kwenye kundi lolote hapo juu, bado unahitaji kuwa na marafiki na hata kuwashawishi marafiki zako(hata mwenza wako) kufanya jambo fulani.
Download kitabu hicho hapa(bonyeza link)
How to Win Friends and Influence People by Dale Carnegie
Kama kuna kitabu chochote unataka sema na utapewa.
Kwa kupata mengi zaidi jiunge na mtandao wa email kwa kubonyeza HAPA na uandike email yako.