Kuna wakati mtu hufikia hatua ya kuona kwamba ili kufanikiwa kwenye maisha ni yeye tu kukomaa na mambo yake. Inafikia hatua mpaka mtu anajiita jeshi la mtu mmoja.

jeshi3

  Kama unajiona wewe ni jeshi la mtu mmoja ama unajihisi unaweza kukomaa mwenyewe kufikia malengo yako basi unahitaji msaada mkubwa sana.

  Kiukweli kwenye mapambano ya maisha hakuna jeshi la mtu mmoja, na hata likiwepo haliwezi kufika mbali. Maadui ni wengi sana kwenye uwanja wa mapambano na mbaya zaidi wana silaha za kutosha kukumaliza mara moja. Kuna changamoto nyingi sana kwenye safari ya maisha, kuna kushindwa, kuangushwa, kukatishwa tamaa, kuchoka na majukumu mengine mengi ambayo huwezi kuyafanya mwenyewe.

vita4

  Ili kuweza kuzishinda changamoto hizo ni lazima uwe na timu yako ambayo itakuwa ya msaada sana kwako. Lazima uwe na watu wa kukuwezesha, kukushauri, kukutia moyo, kukusaidia majukumu yako na pia kukuinua pale unapoanguka.

  Watu wengi wanaingia kwenye matendo maovu kwa kukosa watu wazuri wa kuwaweka kwenye timu zao. Watu wanaiba, wanadhulumu na hata kudiriki kuua kwa kutaka kushinda haya mapambano wenyewe. Mwishowe wanajikuta kwenye wakati mgumu zaidi.

 jeshijeshi2

Hebu fikiri ni nini kinamfanya mtu achukue hatua ya kujiua? Si tunasikia watu wanajiua kila mara? Haya yote yanatokana na kufanya haya mapambano kuwa binafsi, kujifanya jeshi la mtu mmoja. Mtu anapata matatizo anakaa nayo mwenyewe badala ya kushirikisha timu yake(kama hata anayo) mwishowe matatizo yanamwia magumu na kujikuta anaishia kuchukua maamuzi ya kukatisha maisha yake. Hakuna tatizo lolote kubwa inaloweza kukosa suluhisho kama watu watashirikishwa.

  Kama unafikiri wewe ni jeshi la mtu mmoja badili mtizamo wako mara moja kabla hujayaaga haya mapambano kabla ya muda wako. Tengeneza timu ya watu unaowaamini na wanaokuamini. Safari yako ya mapambano itakuwa rahisi sana kwani hakuna litakalokushinda.