Unapokuwa na wazo kubwa la kutengeneza kitu kikubwa kitakachoweza kubadili maisha yako na ya wanaokuzunguka hata ujiandae kwa kiasi gani, kuna wakati mambo yatakuwa magumu sana. Kuna wakati utaona kwamba mambo hayawezekani, ulikosea kuchagua kufanya unachofanya na huwezi kufikia malengo uliyojiwekea. Katika wakati huo hata wanaokuzunguka watakushauri uache kwa kuwa hunufaiki. Wakati kama huo unakuwa mgumu sana kwako na unaelekea kukata tamaa.

  Kabla hujakata tamaa ni vyema ukajua wakati kama huo ndio wakati mzuri sana kwenye maisha yako. Ndio wakati mzuri kwako kujipima kama kweli umejipanga na umejitoa kweli kufikia malengo uliyojiwekea. Wakati kama huo ndio wa kujua kama kweli uko tayari kupata unachotaka kwa gharama yoyote. Ukiweza kuuvuka wakati huo hakuna chochote kitakachowez kukukwamisha tena.

USIKATE TAMAA2

  Kumbuka mafanikio hayaji kwa gharama ndogo, kuna gharama kubwa sana unayotakiwa kulipa ili ufanikiwe. Gharama hiyo lazima uilipe kwenye muda, uvumilivu na kutumia uwezo wako wa hali ya juu. Lazima uwe na ndoto na maono makubwa na lazima uweze kusonga mbele hata unapokutana na vikwazo.

  Habari zote tunazozisikia za watu waliofanya mabadiliko makubwa duniani wote hawakukata tamaa, wote waliendelea kwenda hata mambo yalipokuwa magumu, cha kufurahisha ni kwamba walitoboza, walifanya vitu na vikaonekana.

  Kama na wewe unataka siku moja watu waje wazungumzie mchango wako kwenye maisha ya wengine usikate tamaa. Kila mtu ana mawazo makubwa na mazuri ya kuwanufaisha wengine ila wengi wanakufa na mawazo yao. Furahia kuishi milele, maana unapofanya makubwa hata utapokufa jina lako litaendelea kuwepo milele(soma; sio wote tunaowazika wanakufa)

  Kabla hujakata tamaa ya kuendelea kutekeleza wazo lako kubwa uliloko nalo kumbuka maneno haya;

  “Endelea kwenda mbele, hata mambo yanapokuwa magumu na kila mtu anafikiri huwezi usikate tamaa. Vumilia na kaza mwendo, mwishowe watakuwa wanatangaza mafanikio yako, hiyo ni kama tu hutokata tamaa

 

  Nakutakia mafanikio kwenye harakati zako za kufikia malengo yako.

 

Blog hii imeingizwa kwenye shindano la blogs Tanzania, inashindanishwa kwenye vipengele vitatu BEST INSPIRATIONAL, BEST CREATIVE WRITING NA BEST BUSINESS BLOG. Tafadhali bonyeza hapa kuipigia blog hii kura kwenye shindano la blogs tanzania. Ipigie kura blog amkamtanzania.blogspot.com