Rafiki yangu JOHN GABRIEL alinishirikisha mradi mmoja ambao niliuona ni mzuri sana kwa kila mtanzania. Mradi huo unaitwa VOLUNTEER TZ.
Volunteer Tz ni mradi unaohamasisha watanzania kujitolea kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo kwa ajili ya kuleta maendeleo kwenye nchi yetu. Pia kupitia mradi huu wenye ujuzi mbalimbali wanajitolea kuwafundisha wasio na ujuzi ama uzoefu kupitia madarasa mbalimbali yatakayoandaliwa na mradi.
Ni mradi mzuri sana kwa kila mtanzania kushiriki, kwa wenye ujuzi na uzoefu kutoa na kwa wale wasiokuwa nao kujifunza kutoka kwa wenzao. Pia kupitia mradi huu mbinu mbalimbali za kujiajiri na kufanikiwa kwenye ajira zitatolewa.
Kama tukiweza kuufanikisha mradi huu tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana kama taifa kwa kuchukua hatua na kuacha tu kulalamika.
Kama upo tayari kuwa sehemu ya mabadiliko makubwa kwa maisha yetu na ya wanaotuzunguka tafadhali jiunge na mradi huu sasa. Kwa sasa unaweza kujiunga na mradi huu kupitia Facebook(bonyeza hapa kuingia kwenye kundi la mradi facebook) Ukishaingia kwenye group hilo omba kujiunga(angalia sehemu iliyoandikwa join group) kisha ombi lako litapokelewa na utakuwa mwanachama.
Kuna mipango mingi sana mizuri itakayotekelezwa na mradi huu. Ukishakuwa mwanachama utaiona mipango hiyo.
Pia unaweza kusoma zaidi maelezo ya mradi huo kwa kubonyeza hapa.
Jiunge na mradi huu uwasaidie watanzania wenzako na pia upate msaada kutoka kwa watanzania wenzako.
Hakuna kitu kizuri kama kufanya kitu kinachobadilisha maisha ya watu. Kama tulivyoona kwenye makala ya Kama unafanya ili upate fedha maisha yako yatakuwa magumu sana, wengi wa walioleta mabadiliko makubwa duniani hawakuweka fedha kama lengo lao kuu.
Tamani kubadili maisha ya mtanzania mwenzako kwa ujuzi na uzoefu wowote ulionao. Jiunge na mradi huu na uwe sehemu ya mabadiliko kwa nchi yetu.