1. Nenda kwenye address ya blogger kwa kutumia www.blogger.com
2. Nenda sehemu ya sign in kisha weka username na password
3. Kisha ingia
4. Utakuja ukurasa unaofanana na hii picha
Utahitajika kudhibitisha wasifu wako
5. Utaletewa wasifu wa aina mbili kama inavyoonekana hapo chini
unaweza kuchagua blogger profile ambayo utatumia kwa blogger tu ama ukachagua Google+ profile ambayo itakuruhusu kutumia Google+
Nakushauri utumie Google+ profile ili uweze kushirikisha watu maandiko yako kwenye Google+.
6. Ukichagua Google plus itakutaka ukamilishe profile yako ya Google+
weka taarifa zinazohusika kisha endelea mbele.
Mwisho itakuja sehemu ya kukuruhusu kuendelea na blogger kama inavyoonekana hapo chini
7. Baada ya kubonyeza continue to blogger itakupeleka sehemu ya blogger kama inavyoonekana hapo chini.
Bonyeza NEW BLOG na hapo itakupeleka kutengeneza blog mpya.
8. Kwenye kutengeneza blog kutaonekana hivi;
Kwenye TITLE weka jina unalotaka lionekane kwenye blog yako
Kwenye ADRESS weka anwani itakayotumia kufikia blog yako. wakati unaweka adress wasipokuwekea tiki au wakiweka kosa maana yake hiyo adress inatumika hivyo chagua nyingine. Sio lazima adresss ifanane na title ila ni vizuri kama hazitatofautiana sana.
Baada ya hapo chagua template itakayotumiak kwa blog yako. Kuna templates nyingi sana zinaonekana kwa chini hapo, usihangaike sana kuchagua ni ipi nzuri kwa sasa weka yoyote kwa sababu utaweza kubadili baadae.
Angalia mfano wa uliojazwa;
9. Ukibonyeza CREATE BLOG unakuwa tayari umeshatengeneza blog yako na utaona ukurasa ufuatao;
10. Bonyeza jina la blog yako(kwa mfano kwenye picha hapo juu TENGENEZA BLOGU ndio jina la blog ninayotengeneza).
Ukishabonyeza jina hilo utapelekwa kwenye DASHBOARD ya blog yako ambako ndio kuna kila kitu utakachohitaji kutumia ili kuendesha blog yako.
Dashboard yako itaonekana hivi;
![]()
Kwa kufuatisha namba zilizozungushiwa maduara meusi
1. ni sehemu ya kuanzia kuandika, ukibonyeza hapo unaanza kuandika post
2. ni sehemu inayoonesha takwimu kwa ufupi, watembeleaji.
3. ni sehemu mbalimbali zinazohusika na kubadili blog na kuweka mipangilio
4. inaonesha takwimu kwa ufupi, idadi ya post, idadi ya koment na idadi ya wafuatiliaji
5. ni sehemu inayoonesha notification kama una email au kuna mtu amekoment kwenye blog
6. ni sehemu ya kusign out
7. ni sehemu ambayo ukiibonyeza inakupeleka kwenye blog kama inavyoonekana na msomaji wa kawaida.
Mpaka kufikia hapo tayari unayo blog yako na kilichobaki ni wewe kuanza kupost na kufanya marekebisho machache.
Fuatisha hatua hizi na utengeneze blog yako kama utakwama popote weka maoni hapo chini.