Baada ya kujifunza jinsi ya kutengeneza blog sasa tunakwenda kujifunza jinsi ya kubadili muonekano wa blog.

  Ni muhimu sana blog kuwa na muonekano mzuri na wenye kuvutia. Ili kubadili muonekano huo unatakiwa kubadili template ya blog yako.

 

Sehemu unazoweza kupata template nzuri.

Kabla ya kubadili template, kwanza inabidi udownload template kutoka kwenye mtandao na kuhifadhi kwenye kompyuta yako.

Ili kupata template nzuri tembelea mitandao ifuatayo;

1. http://btemplates.com/

2. http://www.deluxetemplates.net/

3. http://www.mybloggerthemes.com/

4. http://www.bloggerthemes.net/

5. http://www.blogcrowds.com/resources/blogger-templates/

Kuna sehemu nyingine nyingi ambazo unaweza kupata template nyingine nzuri. Katika kila link hapo kuna templates nyingi hivyo chambua mpaka upate nzuri unayoipenda. Ukishapata unayoipenda download na ujue ni sehemu gani umehifadhi kwenye kompyuta.

Mara nyingi hizi template huwa zinakuwa zipped hivyo unatakiwa ku-unzip(kuzifungua).

 

Jinsi ya kuweka template uliyodownload.

1. Nenda kwenye blogger na usign in.

2. Bonyeza sehemu ya tempalate

1.

 

3. Bonyeza BUCKUP/RESTORE

3

 

4. Bonyeza DOWNLOAD ili kuhifadhi tempate yako ya sasa ili kama mambo hayatakwenda vizuri uweze kurudisha template ya zamani.

4

 

5. Baada ya kudownload template ya sasa, bonyeza browse na uchague ulikoweka template ile uliyodownload mwanzo kwa ajili ya kubadilisha.

6. Ukishaichagua bonyeza UPLOAD.

7. Baada ya hapo utakuwa umebadili template yako, marekebisho kidogo kidogo yaliyobakia utaendelea kuyafanya taratibu.