Napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia wasomaji wote wa AMKA MTANZANIA heri ya sikukuu ya pasaka. Kwa wale walioko mapumzikoni kipindi hiki cha sikukuu nawatakia mapumziko mema. Na kwa wale wanaoendelea na shughuli zao pia nawatakia shughuli njema.

pasaka
Kwa wale wanaosherekea sikukuu hizi sherekea vizuri huku ukijua kuna maisha baada ya hizi sikukuu, usisherekee ukapitiliza halafu baada ya sikukuu ukawa katika hali mbaya. Tumia muda huu wa sikukuu na mapumziko kutafakari maisha yako na kuangalia ni wapi ulipo na ni wapi unataka kwenda.
Fanya kitu cha ziada wakati huu wa sikukuu. Ijumaa nilitoa kitabu cha kujisomea kipindi hiki cha sikukuu na nilisema atakayekimaliza kwa siku nne aniandikie nimpe zawadi.
Umekipata kitabu? Umeanza kukisoma? Kama bado hujakipata au kukisoma kitabu hiki fuata maelekezo haya hapa chini;
  Leo nakutumia kitabu kinachoitwa The Power of Self Confidence kilichoandikwa na Brian Tracy. Kama jina linavyojieleza utajifunza umuhimu na nguvu ya kujiamini mwenyewe. Ni ukweli usiopingika kwamba mafanikio yanaanzia na kujiamini wewe mwenyewe. Kama hujiamini ni vigumu sana kupambana na kuchukua fursa mbalimbali zinazokuzunguka.
  Katika kitabu hiki Brian Tracy ameelezea vitu muhimu unavyotakiwa kufanya ili kujijengea kujiamini na kuondokana na hofu. Kitabu hiki kina kurasa 91, ila ukiondoa za utangulizi na za mwisho unabaki na kurasa 60 zenye mafunzo haya. Kwa hiyo kama utakisoma ndani ya siku nne ina maana kwa siku moja unatakiwa kusoma kurasa 15. Kama ukitenga masaa mawili tu kwa siku yanakutosha kusoma kurasa hizo 15 na ukazielewa vizuri.
  Kupata kitabu hichi bonyeza maandishi haya ya jina la kitabu na utaanza kukidownload. The Power Of Self Confidence by Brian Tracy.

Nakutakia kila la kheri katika sikukuu hizi na katika harakati zako za kuboresha maisha yako.
Kumbuka, TUKO PAMOJA