Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutengeneza Pesa Kwenye Mtandao.

Jana jumapili tarehe 20/04/2014 kwenye kipindi cha AMKA NA BADILIKA kupitia TBC1 mada iliyokuwa ikizungumzwa ilikuwa ikihusu mitandao ya kijamii. Wageni walikuwa mwakilishi kutoka TCRA(mamlaka ya mawasiliano) na Bwana Mike Mushi, mmoja wa waanzilishi wa mtandao mkubwa Tanzania unaoitwa Jamii Forums. Walikuwa wakizungumzia changamoto na jinsi ya kunufaika kiuchumi na mitandao ya kijamii.

  Yalizungumzwa mambo mengi sana, lakini moja lililonigusa sana ni kuhusu kutengeneza fedha kupitia blogs. Mike Mushi alisema ni vigumu sana kutengeneza fedha kupitia blog kwa kutegemea matangazo. Inakubidi uwe na watembeleaji wengi sana ndio uweze kushawishi kampuni kubwa iweke tangazo kwenye blog yako. Na hii ndio imekuwa ikisababisha blog kuweka habari zisizo na maadili ili kupata watembeleaji wengi na waweze kupata matangazo. Mwisho wa siku hawapati hayo matangazo na heshima yao inashuka sana.

blog pesa

  Kitu kingine kinachofanya kutengeneza fedha kwenye mtandao kupitia blog kuwe kugumu ni ukosefu wa ubunifu. Kila mtu anayefungua blog siku hizi anaripoti habari. Kwa njia hii kumekuwa na kelele nyingi sana kwenye mtandao kitu ambacho kinawafanya wanaojihusisha na aina hii ya kublog kuumia sana kichwa kutokana na kutopata kile walichodhamiria kupata.

  Pamoja na yote hayo bado kuna nafasi kubwa sana ya kuingiza kipato kisicho na kikomo kupitia blog. Sekta ya utumizi wa mtandao wa internet hapa kwenye Tanzania bado ni ndogo ila inakuwa kwa kasi sana. Bado kuna soko kubwa sana ambalo kama ukiweza kulitumia vizuri unaweza kuanzisha na kukuza biashara yako kupitia mtandao. Huduma za malipo kwa kutumia simu kama mpesa na tigo pesa zimefanya biashara hii kuwa rahisi zaidi.

  Ili kukuondolea adha hii ya kupoteza muda kwenye mtandao kwa kufanya vitu ambavyo haviwezi kukulipa, nimekuandalia kozi fupi ya JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KUPITIA BLOG. Kozi hii itakuwa na vipengele vifuatavyo.

1. Utambulisho wa blog na aina mbalimbali za blog.

2. Njia mbalimbali za kutengeneza fedha kupitia blog.

3. Kuweka misingi ya blog yako na kuchagua mtindo wako.

4. Uandishi wa makala zenye mvuto.

5. Kujenga hadhira na kuvutia wasomaji wengi zaidi(email list).

6. Kuunganisha blog na mitandao mingine ya kijamii ili kupata wasomaji wengi zaidi.

7. Kuchagua njia ya kuingiza fedha kutumia blog.

8. Uandishi wa makala za kuuzia bidhaa au huduma na siri iliyoko nyuma ya utafutaji wa masoko.

9. Kutengeneza fedha kusiko na kikomo kupitia blog yako.

10. Kutofautisha blog yako na blog nyingine na jinsi ya kuendelea kuikuza zaidi.

  Kozi hii itafundishwa kwa njia ya mtandao na itachukua muda wa siku kumi tu. Gharama ya kozi hii ni shilingi elfu kumi za kitanzania.

  Kujiunga na kozi hii tuma fedha(tsh 10,000/=) na email yako kwa mpesa au tigo pesa 0755953887/0717396253 kisha utaingia kwenye kozi hii. Kozi itaanza rasmi tarehe 28/04/2014. Mwisho wa kujiunga na kozi hii ni ijumaa ya wiki hii tarehe 25/04/2014.

  Wahi kujiunga na kozi hii kabla muda haujaisha. Hatutapokea watu katikati ya kozi.

  Hii ni nafasi kubwa sana kwako kuweza kutengeneza kipato cha uhakika na kisicho na kikomo. Dunia inabadilika kwa kasi sana na mtandao wa internet umetengeneza matajiri wengi sana duniani. Usiachwe nyuma na njia hii ya kipekee na ya uhuru ya kujiingizia kipato.

  Karibu kwenye ukombozi wa maisha yako kiuchumi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: