MAKALA HII IMEANDIKWA NA JOHN MATIKU

KIMSINGI mafanikio yapo yanaishi, nasi tunaishi nayo ila mgangano mkubwa ambao unatoa matokeo ya maisha magumu kwa watu ni utendaji duni wa  mifumo.

Kwa kawaida nguzo ya wabunifu wote nikutengeneza mfumo unaofanyakazi ili kutoa matokeo wayatakayo.

Mfano …wabunifu wa mfumo wa utawala hawa kwa kiwango kikubwa hawakukosea wakati wakuunda mfumo chukulia mfano wa utawala wa hapa kwetu Tanzania.

Tunayo serikali kama mtendaji, Tuna Bunge kama msimamizi wa mtendaji (Serikali) pia  tunayo Mahakama kama msimamizi mkuu wa haki na uwajibikaji. Huu ni mfumo tayari ambao unatakiwa kutenda kazi na kupeleka mbele gurudumu la maendeleo.

Lakin muda mwingine maendeleo hayapatikan!  Mara nyingi si kwa sababu mfumo ni mbaya la hasha! Bali mfumo unakawaida ya kutenda kazi chini ya kiwango!

MAFANIKIO2

Hamishia sasa mfano huu kwenye maisha yako halisi! Chukua kitu unachokifanya saizi kama maisha yako. Iwe ni kazi kwa maana ya kwamba wewe ni mfanyakazi, iwe masomo kwa maana ya kwamba wewe ni mwanafunzi, iwe ni biashara au shughuli yoyote ile. Umekua ukifanya na kupata matokeo flani. Matokeo yanaweza kuwa mazuri, si mazuri sana wala si mabaya, au hata mabaya!

Hapa kwenye matokeo ya tunachokifanya ndipo utasikia watu tukibagua! Wengne utasikia wanasema biashara flan hailipi! Kwa ajili ya matokeo aliyo yapata huko au masomo flani magumu sana sababu ya matokeo aliyopata yeye!

Kimsingi hapa ndipo shida ilipo watu wengi hatuangalii UTENDAJI WA MFUMO Badala yake tunahangaika na Matokeo!

Ziko njia nyingi na baadhi zinafundishwa sana humu AMKA MTANZANIA za jinsi gani unaweza kwenda zaidi ya mfumo uliopo na ukapata mafanikio makubwa zaidi badala ya kukaa na kujilau au kuwalaumu watu wengne kwa matokeo yaliyopatikana.

Mfano wewe ni mkulima na  unalima kwa kutegemea majira! Mvua zikianza unalima unapanda unapalilia, inaendelea kunyesha mpaka unakomaza mazao na kuvuna huo ni mfumo wa kiasili. Lakini ili upate mazao zaidi fikiria kuwa na mitambo ya umwagiliaji japo ya bei ndogo kwanza, ili hata mvua isiponyesha kwa wakati uweze kupata mazao. kumbuka Usipoenda zaidi iko siku utaulaumu mfumo tu!

Hivyo hivyo mashulen umeenda shule kusoma ni sawa kabisa, lakini mfumo uliopo unatenda kazi chini ya kiwango japo lengo ni kufundishwa ili ufaulu, bado huwezi faulu vizuri kwa kuutegeme mfumo uliopo. Badala yake nenda zaidi ya mfumo tafuta muda na jinsi ya kujisomea mwenyewe.

Hata kwenye biashara pia pamoja na ubunifu wako lakin tayari uko kwenye mfumo flani hata kama unapata matokeo mazuri si wakati wa kulala na kustarehe lazima ufikili kwenda zaidi ya mfumo kwa maan ya kuboresha zaidi, ili upate matokeo makubwa na mazuri zaidi.

MWISHO
Nimalize kwa kusema tumezaliwa kuwa WASHINDI ila ziko GHARAMA za kulipa ili kuwa MSHINDI na unazimudu.

Uchaguzi ni wako utalipa GHARAMA Ili uishi kama MSHINDI au utalegea uishe kama aliyeshindwa.

Asante.

UNAWEZA KUWASILIANA NA MWANDISHI WA MAKALA HII JOHN MATIKU KWA johnmatiku1@gmail.com

KAMA NA WEWE UNA MAKALA NZURI ULIYOANDIKA NA UNAFIKIRI INAWEZA KUWAAMSHA WATANZANIA TAFADHALI NITUMIE KWENYE amakirita@gmail.com

MAKALA ISIWE IMEWEKWA KWENYE BLOG AU CHOMBO KINGINE CHA HABARI, IWE IMETUMIA KISHWAHILI RAHISI NA KINACHOELEWEKA NA IWE NA MANENO KATI YA 500 NA 1000 KARIBU SANA.