Sababu Sita Ambazo Watu Wanaotaka Mafanikio Huwa Nazo

MAKALA HII IMEANDIKWA NA IMANI NGWANGWALU WA TANGA TANZANIA.

Siri ya mafanikio mara nyingi huwa inategemea namna unavyojijengea mkabala wa mafanikio katika maisha yako. Kuna nadharia nyingi au kanuni za kwa namna gani binadamu anaweza kupata kile anachokihitaji maishani.Nadharia au Kanuni mojawapo ni KANUNI YA KUPATA KILE UNACHOHITAJI KATIKA MAISHA hii utajifunza katika makala nyigine zinazofuata katika mtandao huu. Pamoja na nadharia hizo na mikabala hiyo pia zipo sababu ambazo watu wanaotaka mafanikio huwa nazo, sababu hizo ni kama ifuatavyo:-

1. UBINAFSI, hii ni tabia inayomwezesha mtu kufanya maamuzi yanayozingatia matokeo atakayo. Na sio ile tabia ya kitoto unayoijua wewe ya changu ni changu siyo hiyo. Ubinafsi unaozungumzwa hapa ni wa kulenga au kuhitaji matokeo fulani unayoyataka. Unapokuwa mbinafsi unakuwa na tabia ya kuuliza namna ya kutumia muda, nishati na pesa ili vitu hivyo vikusogeze katika lengo. Ni vigumu kuwa mbinafsi pasipo kujua aina ya maisha unayotaka kuishi.

Kitu unachotakiwa kujifunza ni kuchagua aina ya maisha unayotaka kuishi na unapojifunza kuchagua aina ya maisha unayotaka kuishi ndio hivyo unakuwa mbinafsi. Watu wengi sana sio wabinafsi kwa sababu hawana uchaguzi mzuri wa maisha ,matokeo yake wanakuwa ni watu wa matatizo siku zote. Kwa mfano takwimu zinaonyesha kati ya watu 100 ni watu watatu au wanne tu ambao ni wabinafsi nikiwa na maana kwamba hawa ndio wenye uchaguzi halisi ikiwa ni pamoja na kupanga malengo na kuyatimiza. Mimi sijui wewe uko wapi ? Kuwa mbinafsi ni tabia ya watu wachache Sana! Kwanini wewe usichukue tabia hii ili ikuwezeshe kuishi maisha unayoyataka? Kama unataka kuwa mbinafsi sahau kwanza kuishi maisha wanayoishi watu wengine maana si kila mtu anataka kufika unakotaka kwenda.

MAFANIKIO2

2.NGUVU YA MWELEKEO. Ni ngumu sana kuwa na nguvu ya mwelekeo kama hujui unakoelekea. Bila mitazamo makini huwezi kuwa na nguvu ya mwelekeo kwenye matokeo unayo yahitaji. Ni rahisi sana kupumbazwa, kukosa mpangilio na kupoteza msimamo. Nguvu ya mwelekeo(Nguvu ya uzingativu) zinakuwa na madhara makubwa sana na ya faida katika kukufanikisha. Na ninaposema nguvu ya mwelekeo kama bado hujanielewa vizuri ni nguvu ya kushikilia kitu kimoja au kung’ang’ania lengo moja mpaka uone matokeo.

3. NIDHAMU, kama umeamua kuzifikia ndoto zako lazima uwe na kitu kinachoitwa nidhamu, hii ni tabia ya kufundishwa pia inatokana na udhibiti binafsi. Kuwa na nidhamu maanake ni kwamba hutayaacha malengo yako, kwa vile unajenga maisha unayoyataka, basi nidhamu ni zana muhimu sana.  Nidhamu inakufundisha kuwa maisha sio tambarare, yana miinuko na uzoefu unakufundisha kuwa ukiwa na maisha ya nidhamu unaweza kupita kwenye miinuko hiyo.

4.UNG’ANG’ANIZI, ni hali ya kuendelea na matokeo fulani bila kukata tamaa. Malengo yako yanafahamika,una dira,una nidhamu na ni mbinafsi lakini unakutana na vikwazo. Haja tu ya kutaka kuendelea hukufanya uvione vikwazo hivi kama nafasi badala ya tatizo.

Hata hivyo kama ingekuwa rahisi, basi kila mtu angefikia hapo ulipo,  lakini si kila mtu yupo kwenye uwanja wa vita pamoja nawe. Wengi sana huwa wanasimama pindi wakutanapo na vikwazo. Wewe unaona vikwazo na kuona nafasi papo hapo. Unajua unakoenda na unajua huwezi kuzuiliwa na kitu chochote. Ung’ang’anizi wako ndio unaokuvuta mbele. Unatafuta njia penye kizuizi chochote.

5. UMILIKI, hii ni hali ya mmiliki. Ni kuchukua haki ya kumiliki kitu. Hapa ni ndoto zako,malengo na maisha yako. Usipochukua jukumu la kuzimililki ndoto zako mwenyewe, ni nani atafanya hivyo? Jifunze kumiliki ndoto zako matokeo yake utaona kwani kila ukitendacho kitafanikiwa na utapata matokeo uyatakayo.

Mara nyingi huwa tunatumaini mema wakati unapanga kwa mabaya. Kweli uko tayari kwa chochote unachopewa na haya maisha? Unapochukua umiliki ni kufanya mabadiliko ya kukusaidia kukupeleka mbele, kubadili tabia zisizo na tija, labda hata kubadili marafiki wasioeleweka, kushugulika na dunia kadri ilivyo na sivyo wewe unavyotaka iwe. Kama huna mbinu za kumiliki unaweza ukamwona mwingine akufundishe.

6.KUPIMA MATOKEO, Siyo jambo dogo matokeo yanatakiwa kuwepo katika hali fulani ambayo wewe mwenyewe umepanga. Uliweka malengo na matokeo uyatakayo,ulipanga unavyotaka mambo yaishie na kwa vile unaumiliki, nguvu ya mwelekeo, na nidhamu na fahamu kuwa una mbinu, msukumo,tama na uelewa na tayari una ramani inayokuelekeza pa kwenda. Matokeo na kupima ni kupima njia ya mafanikio. Hakuna visingizio,hakuna kujuta, ni matokeo tu,hakuna kujaribu bali kufanya tu. Mambo yanapoharibika hakuna kusononeka ni kuwajibika tu ndiko kunakotakiwa.

Kwa kifupi hizi Ni baadhi ya sababu ambazo watu wanaotaka mafanikio huwa nazo na wewe pia unaweza ukajifunza na kusonga mbele zaidi ya ulipo, nakutakia kila la Kheri katika safari ya maisha.

 

UNAWEZA KUWASILIANA NA MWANDISHI WA MAKALA HII IMANI NGWANGWALU KWA 0767048035.

KAMA NA WEWE UNA MAKALA NZURI ULIYOANDIKA NA UNAFIKIRI INAWEZA KUWAAMSHA WATANZANIA TAFADHALI NITUMIE KWENYE amakirita@gmail.com

MAKALA ISIWE IMEWEKWA KWENYE BLOG AU CHOMBO KINGINE CHA HABARI, IWE IMETUMIA KISHWAHILI RAHISI NA KINACHOELEWEKA NA IWE NA MANENO KATI YA 500 NA 1000 KARIBU SANA.

2 thoughts on “Sababu Sita Ambazo Watu Wanaotaka Mafanikio Huwa Nazo

 1. Felix .K. May 7, 2014 / 8:56 pm

  Hbr za saa hizi? Ukitumia makala inayokidhi vigezo ulivyoeleza hapo juu, kuna malipo yo yote unayompa mtumaji?

  Like

 2. Makirita Amani May 8, 2014 / 4:55 pm

  Habari Felix,
  Hakuna malipo yoyote nayotoa kwa sasa kwa wanaotuma makala. Ila hii inawasaidia kuongeza utembeleaji wa blog zao kwa wale ambao wana blog maana kwenye makala yake kunakuwa na link ya blog yake. Kwa kuwa AMKA MTANZANIA inaweza kuwa na wasomaji wengi na ambao hawaijui blog ya mwandishi huyo wanaweza kuijua na kuwa wasomaji wa kudumu kutokea kwenye makala iliyowekwa hapa. Karibu.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s