Kama unavyojua kwamba ni muhimu sana kutengeneza email list kwa ajili ya kujenga uhusiano mzuri na wasomaji wako. Na kwa wale waliosoma kozi ya JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG tulijadili vizuri umuhimu wa email list na jinsi gani unaweza kupata watu wengi wanaojiunga na email list yako.
Leo nitatoa maelekezo ya namna unavyoweza kuweka autoresponder kwenye blog yako.
Kuna autoresponder nyingi za bure na nyingine za kulipia. Mimi binafsi nimewahi kutumia autoresponder mbili kwenye kutengeneza email list.
Ya kwanza ilikuwa LISTWIRE, ambayo ni nzuri na ni bure kabisa na ya pili ni MAIL CHIMP ambayo kuna bure na kuna kulipia.
Kati ya hizi mbili nimeipenda zaidi mail chimp na ndio nitaielekeza hapa.
Kwanza kabisa kwenye mail chimp kuna bure na kulipia, bure unaweza kuwa na list yenye watu mpaka 2000 na kutuma email 12,000 kwa mwezi mmoja. Ni rahisi sana kutumia na unaweza kuweka vitabu na watu wakadownload moja kwa moja wanaposoma email unazowatumia. Pia unaweza kupanga email iende kwa wasomaji saa ngapi(yaani kuschedule).
Jinsi ya kuweka autoresponder kwenye blog yako hatua kwa hatua;
1. Nenda http://mailchimp.com/ utaona kama picha hapo chini;
2. Bonyeza palipoandikwa SIGN UP FREE, itakuja picha kama hapo chini,
3. Weka email yako, jina unalotaka kutumia na password. Kisha bonyeza CREATE MY ACCOUNT.
4. Nenda kwenye email yako na udhibitishe akaunti yako uliyotengeneza. Bonyeza ACTIVATE ACCOUNT
5. Utadhibitisha kama wewe ni binadamu kwa kuandika maneno utakayooneshwa.
6. Baada ya hapo weka majina yako, kwenye organisation informatio chagua taarifa husika kulingana na wewe, kwenye name of organisation weka jina la blog na kwenye website url weka url ya blog yako weka sanduku la posta kwenye adddress one kisha bonyeza SAVE AND GET STARTED. Hakikisha kila sehemu imejazwa la sivyo itakataa kuendelea mbele.
7. Baada ya kusave itakupeleka kwenye DASHBOARD kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.
8. Bonyeza start building your AUDIENCE bonyeza mbele palipoandikwa create list. Baada ya kufunguka bonyeza juu kulia palipoandikwa create list, itaonekana kama picha hapo chini.
9. Jaza taarifa zote zinazohusika hapo. Weka jina la list, email yako ambapo utakuwa unapokea majibu, taarifa fupi ya kumkumbusha msomaji alijiungaje na list unaweza kuweka na namba yako ya simu. Zip code weka 255, baada ya hapo bonyeza daily summary na kisha SAVE.
10. Baada ya hapo itarudi kwenye dash board. Bonyeza SIGN UP FORM kama inavyoonekana hapo chini.
11. Bonyeza embeded forms kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.
12. Baada ya kubonyeza hapo utapata picha kama zinavyonekana hapo chini.
Hapo juu kushoto kwenye SUBSCRIBE TO OUR EMAIL LIST weka maeneno yako ya kumvutia mtu ajiunge. Baada ya hapo copy hayo maandishi palipoandikwa COPY/PASTE ONTO YOUR SITE, ukibonyeza tu katikati yanajihighlight. Yakopi.
13. Nenda kwenye blogger, bonyeza LAYOUT na kisha bonyeza sehemu ya juu kulia palipoandikwa ADD GADGET, kama inavyoonekiana hapo chini.
14. Zitakuja gadget nyingi chagua HTML/JAVA SCRIPT kama inavyoonekana hapo chini.
15. Baada ya kufunguka paste yale uliyokopi kwenye sehemu iliyoandikwa contents kisha save.
16. Baada ya hapo utakuwa umekamilisha na itaonekana kwenye blog yako kama picha inavyoonesha hapo chini.
Kujua watu waliojiunga na email list yako nenda kwenye mail chimp log in na utaona taarifa zote.
Kuwatumia wasomaji wako makala au ujumbe wowote kwa autoresponder nenda kwenye mail chimp kisha bonyeza sehemu ya CAMPAIGN kisha bonyeza CREATE CAMPAIGN.
Yaliyobaki ni kufuata maelekezo tu.
Karibu sana.