Katika dunia ya sasa hakuna kitu muhimu kama kujisomea na kujifunza mambo mapya kila wakati. Hii ni njia moja ya uhakika ya kuwekeza ndani yako na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufanikiwa kwenye kile unachofanya. Kujisomea kunakupatia maarifa, kunakuongezea uwezo wa kufikiri na kunakuwezesha kupambana na changamoto unazokutana nazo kwenye maisha ya kila siku. Pia kujisomea kunakuletea furaha na kukuepusha na msongo wa mawazo unaotokana na changamoto za maisha.

KUJISOMEA2

Pamoja na kujua yote haya lakini bado ni wachache sana wanaoweza kujisomea na kujifunza mambo mapya na yanayohusiana na shughuli wanazofanya. Wengi tunafikiri kusoma kunaisha pale tunapohitimu masomo yetu, hili ni kosa kubwa sana na linakuzuia kufikia mafanikio makubwa.

Mara kwa mara nimekuwa nikituma vitabu vizuri kwa wasomaji wa AMKA MTANZANIA, je ni vitabu vingapi ulivyopokea na ukavisoma? Nina uhakika kama umepokea vitabu vitatu basi hata kimoja bado hujamaliza kukisoma. Unaweza kuwa na nia ya kweli ya kujisomea ila kila unapotaka kusoma unapata sababu ya kutosoma wakati huo na hivyo kusogeza mbele.

Kama hali hii inakutokea usiumie sana, kwa sababu kwa nafasi kubwa sio kosa lako na pia sio rahisi kama unavyofikiri. Kujisomea ni tabia ambayo inatakiwa kujengwa ili iwe sehemu ya maisha yako na isikusumbue sana unapotaka kufanya hivyo.

Kutokana na umuhimu huu wa kujisomea na kutokana na wengi kushindwa kujijengea tabia ya kujisomea mwezi wa sita ndani ya KISIMA CHA MAARIFA tutajifunza jinsi ya kujijengea tabia ya kujisomea. Kwa wiki nne, kila wiki utapata makala moja yenye mafunzo jinsi ya kujenga tabia hii muhimu ya kujisomea na mbinu mbalimbali za kuiboresha na kuifanya idumu. Pia kutakuwa na mazoezi ya kufanya ili kuiboresha tabia hii na kufanya iwe sehemu ya maisha yako.

Hiki ni kitu muhimu sana kwenye maisha yako ambacho hutakiwi kukikosa. Kwa wale ambao tayari ni wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA wataendelea kupata mambo haya mazuri kila mwezi. Kama bado hujawa mwanachama wa kisima, jiunge sasa ili na wewe uweze kupata mambo haya mazuri ambayo yataboresha maisha yako kwa kiwango kikubwa sana.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma fedha tsh elfu kumi(10,000/=) kwa mpesa-0755953887 au tigo pesa-0717396253 na kisha tuma email yako kwa meseji kwenye moja ya namba hizo na utaunganishwa kwenye kisima cha maarifa.

Kumbuka utaratibu wa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA umebadilika hivyo unaweza kujiunga siku tatu za mwisho wa mwezi. Kwa mwezi huu unaweza kujiunga leo tarehe 28, 29 na tarehe 30. Ukikosa kujiunga katika siku hizi tatu itakubidi usubiri mpaka tena tarehe za mwisho wa mwezi unaofuta.

Chukua hatua leo hii ili usikose nafasi hii adimu ya kubadili na kuboresha maisha yako.

Kumbuka hakuna kitu muhimu kama tabia ya kujisomea na kujifunza. Kama unafanya biashara au kazi na kila siku unakazana kuikuza lakini haikui basi jibu lako ni moja tu, unahitaji kukua wewe kabla biashara yako haijakua.(soma; hii ndio sababu kubwa kwa nini biashara yako haikui)

Jiunge na kisima cha maarifa sasa ili uweze kujifunza tabia hizi muhimu za kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa. Chukua hatua leo kabla nafasi hii haijapita. Kumbuka una siku tatu tu za kuchukua hatua.

Karibu sana na nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kuboresha maisha yako.

Kumbuka TUKO PAMOJA.