Pamoja na kwamba mambo yamebadilika sana hasa kwenye zama hizi za sayansi na teknolojia, kuna wafanyabiashara wengi sana ambao bado wameshikilia imani za kishirikina au uchawi katika biashara. Moja ya imani hizo ni kitu kinaitwa CHUMA ULETE.

Kama hujui CHUMA ULETE, maana yake ni kwamba wewe unachuma halafu unampelekea mwenzako bila ya wewe mwenyewe kujua. Yaani kuna wafanya biashara wanaamini kwamba hawapati faida kwenye biashara zao kwa sababu kila wanapochuma kuna mtu wanampelekea bila kujijua. Hivyo fedha zinatoka kwao na kwenda kwa mtu mwingine kwa njia ya uchawi.

Imani hii ni kali sana kwa baadhi ya watu kiasi kwamba wanaweza kuepuka kufanya biashara na mtu anayehisiwa kuwa chuma ulete. Kwenye mtaa ninaoishi kuna mzee mmoja akienda maduka ya hapa mtaani hawamuuzii kabisa. Ukiwauliza wanakwambia huyo mzee ni chuma ulete.

Kuna wafanyabiashara wengine wana imani kali sana kuhusu chuma ulete kiasi kwamba ukienda na fedha kubwa asubuhi inayohitaji kurudishiwa chenchi yuko radhi asikuuzie unachotaka. Wanaamini kwamba wanapokurudishia fedha asubuhi hiyo hasa kama ni mteja wa kwanza basi mauzo yote ya siku hiyo yatakwenda kwako. Hii imewahi kunitokea nilienda dukani asubuhi na shilingi elfu kumi kutaka mahitaji, muuzaji akaniambia hana chenchi, nikamwambia nipe mahitaji halafu chenchi nitafuata baadae, alichokifanya alipokea fedha yangu na kuiweka pembeni kabisa, hakuichanganya na fedha nyingine.

Tabia na imani hizi zimenifanya nifikiri sana juu ya hii CHUMA ULETE na kwa nini watu wanateseka kiasi hiki. Swali kubwa nililojiuliza ni je chuma ulete wapo? Kwa kuwa mimi naamini katika sayansi jibu la moja kwa moja lilikuja kwamba hakuna chuma ulete ila ni imani tu za watu. Na kama ilivyo kwenye kila imani, wanaoamini wanaona matokeo ya imani zao.

Baada ya kuja kufikiri kwa kina niligundua sikuwa sahihi kusema chuma ulete hayupo. Ukweli ni kwamba kwenye kila biashara CHUMA ULETE wapo/yupo na kwa bahati mbaya ni vigumu sana kumjua na kumzuia. Ugumu huu unatokana na ukweli kwamba chuma ulete wa biashara yako ni wewe mwenyewe. Unaweza kuhangaika sana kuzuia chuma ulete lakini hujui wewe mwenyewe ndio chuma ulete mkubwa wa biashara yako.

Mahesabu na matumizi yako mabovu ya fedha kwenye biashara ndio yanakufanya uwe chuma ulete wa biashara yako mwenyewe.

Unawezaje kumdhibiti chuma ulete huyu mbaya(wewe mwenyewe) kwenye biashara yako?

Uzuri ni kwamba unaweza kumdhibiti chuma ulete huyu ambae ni wewe mwenyewe kama utafuata misingi muhimu ya mipango na matumizi ya fedha za biashata. Hapa nitaeleza vitu vitano muhimu unavyotakiwa kuvifanya au kuacha kuvifanya ili kumdhibiti chuma ulete na biashara yako iweze kustawi.

1. Tenganisha matumizi ya biashara na matumizi yako binafsi.

Moja ya kosa kubwa linalofanywa na wafanyabiashara wengi na linawaletea upotevu wa hela kwenye biashara zao ni kuchanganya matumizi binafsi na matumizi ya biashara. Ni vigumu sana kuona faida na ukuaji wa biashara kama fedha ya matumizi yako binafsi inatoka moja kwa moja kwenye fedha ya biashara. Utaona unauza sana lakini fedha huzioni, hii ni kwa sababu chuma ulete wewe, unaendelea kutoa fedha za mauzo na kutumia kwenye matumizi yako binafsi. Ili uweze kuona ukuaji halisi wa biashara yako tenga fedha za biashara na fedha za matumizi binafsi.

kitabu kava tangazo

2. Jilipe mshahara kutoka kwenye biashara yako.

Najua unajiuliza sasa nitaishijekama siwezi kuchanganya matumizi ya biashara na matumizi binafsi wakati biashara ndio shughuli inayoniingizia kipato cha kuendesha maisha. Ili uweze kuwa na mtemgano mzuri kati ya fedha ya matumizi binafsi na matumizi ya biashara jilipe mshahara. Unaweza kuamua kujilipa mshahara kwa siku, wiki, au mwezi. Baada ya kujilipa mshahara wako usiguse tena fedha ya biashara, hili linahitaji nidhamu ya kutosha. Njia nzuri ya kujipangia mshahara ni kujilipa kamisheni, yaani unajilipa asilimia fulani ya faida unayopata kwenye biashara. Utakapohitaji kupata mshahara mkubwa zaidi utasukumwa kufanya biashara zaidi ili upate faida kubwa na baadae kamisheni kubwa. Kama biashara unayofanya ndiyo unayotegemea kuendesha maisha yako ningependekeza ujilipe mshahara kwa wiki au mwezi, ukijilipa kwa siku unaweza usione tofauti ninayozungumzia hapa.

Kuendelea kusoma vitu vitatu muhimu unavyotakiwa kufanya ili kuimarisha biashara yako jiunge na KISIMA CHA MAARIFA.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma fedha tsh elfu kumi(10,000/=) kwa mpesa-0755953887 au tigo pesa-0717396253 na kisha tuma email yako kwa meseji kwenye moja ya namba hizo na utaunganishwa kwenye kisima cha maarifa.

Ndani ya kisima cha maarifa mwezi wa sita tutakuwa tunajenga tabia ya kujisomea ambayo ni moja ya tabia muhimu sana ili kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Jiunge sasa na KISIMA CHA MAARIFA ili kupata mambo haya mazuri.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio.

TUKO PAMOJA.