Kila mwezi ndani ya KISIMA CHA MAARIFA tunajadili tabia moja muhimu ya kujenga ili kuweza kufikia mafanikio makubwa katika maisha. Sehemu kubwa ya mafanikio yetu inatokana na tabia zetu ambazo zinatokana na matendo yetu ambayo ni zao la mawazo yetu. Kupitia sehemu hii ya TABIA ZA MAFANIKIO tunajadili jinsi ya kubadili mawazo yetu ili kujenga matendo bora na tabia bora za kukuwezesha kufanikiwa kwenye maisha yako.
Mwezi wa tano tulijadili tabia ya kutunza muda, hapa tuliona ni jinsi gani tunapoteza nusu ya muda wa maisha yetu bila ya sisi wenyewe kujua. Mwezi wa sita tulijadili tabia ya kujisomea, sina haja ya kukuambia ni jinsi gani ilivyo muhimu kuwa na tabia ya kujisomea. Kwa kifupi kama unapenda kujisomea na kujifunza utafanikiwa na kama huna tabia hiyo tayari umeshaaga mashindano(kama tukichukulia mafanikio kama mchezo).
Mwezi wa saba tutajadili tabia muhimu sana ili kuweza kufikia mafanikio. Tabia hii ndio inawashinda zaidi ya asilimia 90 ya binadamu wote duniani. Ni tabia ambayo imekuwa ngumu sana kwa watu wengi kuweza kuitengeneza na kufaidika kwa kuwa nayo. Tabia hiyo ni utengenezaji, matumizi na utunzaji mzuri wa fedha zako binafsi. Hofu kubwa ya watu duniani ni fedha, kila sehemu ya maisha yetu imeathiriwa na fedha.
Pamoja na kwamba fedha ni muhimu sana kwenye maisha yetu lakini bado ndio tuna tatizo kubwa sana kwenye kuelewa sayansi yake. Mwezi huu wa saba tutajadili kwa kina tabia muhimu unayotakiwa kujenga ili kuweza kuwa na matumizi mazuri ya fedha na kuweza kufanikiwa. Kutokana na umuhimu mkubwa wa tabia hii ya matumizi ya fedha, tunaweza kwenda kwa miezi miwili kwenye tabia hii.
Fedha ni muhimu sana kwenye maisha yetu lakini tuna elimu ndogo sana kuhusu fedha. Watu wengi wangependa kuanzisha biashara ila kisingizio kikubwa ni mtaji. Wapo wengine ambao wanapenda kipato chao kiongezeke ila kila kinapoongezeka hawaoni mabadiliko yoyote. Asilimia kubwa ya wafanyakazi mishahara yao haikutani, yaani mshahara wa mwezi mmoja unaisha kabla hajapata mshahara wa mwezi unaofuata. Na wakati mwingine mtu unakuwa na madeni mengi zaidi hata ya kipato chako.
Mambo haya yote tutayajadili kwa kina katika kujenga tabia hii muhimu ya matumizi ya fedha ili kuweza kufikia mafanikio.
Kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA fanya hivyo mara moja ili usipitwe na mambo haya mazuri. Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma fedha tsh elfu kumi(10,000/=) kwa mpesa 0755953887 au tigo pesa 0717396253 na kisha tuma email yako(email ya GMAIL ni nzuri zaidi) na utaunganishwa na kisima cha maarifa.
Kwa kujiunga na kisima cha maarifa utaweza kujifunza tabia zilizopita, kujifunza kutengeneza blog kwa picha na pia kupata mafunzo muhimu ya biashara. Chukua hatua ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA sasa kabla ya muda huu mfupi wa kujiunga haujaisha.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio,
TUKO PAMOJA.
