Hakuna anayeweza kukataa kwamba ili kupata maendeleo na kufanikiwa kifedha kwenye maisha uwekezaji ni muhimu sana. Iwe umeajiriwa, umejiajiri au unafanya biashara ni lazima uwekeze ili uweze kufikia mafanikio makubwa.
Linapokuja swala la uwekezaji kila mtu huwa anakimbilia kuuliza au kujiuliza awekeze wapi. Katika kujiuliza huku ndio mtu anajikuta anapata majibu mengio ambayo yanamuacha njia panda.
Unafikiria uwekeze kwenye kilimo, lakini bado unaona kuna changamoto nyingi. Unafikiria uwekeze kwa kununua hisa au vipande lakini bado unaona mafanikio yanaweza kuwa kidogo sana. Kwa hali hii unajikuta upo njia panda na kushindwa kufanya maamuzi sahihi.
Unapokuwa kwenye hali hii ni rahisi sana kuchukua ushauri wowote kutoka kwa mtu na kuutumia bila ya kufanya uchunguzi wa kutosha.
Leo nataka nikushirikishe uwekezaji muhimu sana ambao kila mtu mwenye kutaka maendeleo na mafanikio lazima aufanye. Narudia tena, LAZIMA UFANYE uwekezaji huu kama kweli unataka kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Uwekezaji ninaokuambia ni uwekezaji wako binafsi. Ni muhimu sana kwako kuwekeza kwenye maendeleo yako binafsi. Uwekezaji huu unaufanya kwa kujifunza na kupata elimu kuhusu maisha, mafanikio, biashara na mengine mengi.
Unawezaje kufanya uwekezaji huu?
Unaweza kufanya uwekezaji huu kwa kujifunza sehemu mbalimbali. Siku hizi imekuwa rahisi sana kujifunza kwani mtandao wa intanet umerahisisha sana upatikanaji wa taarifa. Ila pia mtandao huu wa intanet una taarifa nyingi sana ambazo sio sahihi na zinaweza kukupoteza.
Unaweza kujifunza kwa kusoma vitabu vizuri ambavyo vitabadili mtazamo wako na maisha yako kwa ujumla. Kama hujapata vitabu vitatu ninavyotoa(think and grow rich, rich dad poor dad na the richest man in babylon) nitumie email kwenye amakirita@gmail.com kisha nitakutumia vitabu hivyo.
Unaweza kujifunza kwa kusikiliza vitabu vilivyosomwa yaani AUDIO BOOKS. Hii ni njia rahisi sana ya kujifunza hasa kwa wale ambao hawana muda wa kusoma vitabu au ni wavivu wa kujisomea. Vitabu hivi unaweza kusikiliza ukiwa kwenye foleni au ukiwa katika hali ambayo unaweza kuwa unapoteza muda. Kupata vitabu hivi vilivyosomwa bonyeza maandishi haya.
Kuna njia nyingine bora sana ya wewe kujifunza kila siku. Njia hii ni wewe kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kupitia KISIMA CHA MAARIF utapata nafasi ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu mafanikio na maisha. Utajifunza jinsi ya kujenga tabia za mafanikio, utajifunza juu ya biashara na uwekezaji na pia utakuwa unapata uchambuzi wa vitabu vizuri vinavyoweza kubadili maisha yako.
Utayapata yote haya na mengi zaidi kwa kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA. Ili kujiunga tuma fedha tsh elfu kumi kwenye namba 0717396253/0755953887 na kisha unatuma email yako na unaunganishwa na KISIMA CHA MAARIFA.
Hii ni nafasi ya kipekee kwako kujifunza kwa njia rahisi na kupata mbinu bora za kuweza kufikia mafanikio kwenye maisha yako.
Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA sasa, ifikapo mwezi wa nane gharama ya kujiunga na KISIMA itaongezeka na kufikia tsh elfu ishirini. Wahi nafasi hii.
Kwa vyovyote vile utakavyofanya hakikisha uwekezaji wako binafsi ndio yambo la kwanza unalofanya. Kwani unapokuwa na elimu na taarifa sahihi ndio unaweza kufanya maamuzi sahihi kuhusu uwekezaji gani mwingine ufanye. Huna sababu ya kushindwa kufanya uwekezaji kwako binafsi.
Nakutakia kila la kheri katika uwekezaji wa kuboresha maisha yako.
TUKO PAMOJA.
