Katika uchambuzi wa kitabu cha RICH DAD POOR DAD unaoendelea kwenye KISIMA CHA MAARIFA kuna mambo mengi sana ambayo tumeendelea kujifunza kuhusu elimu ya fedha. Kila mmoja wetu anapenda kuwa na uhuru wa kifedha au kuwa tajiri. Lakini watu wengi wanaishia kuwa na maisha magumu licha ya kufanya kazi kwa bidii na juhudi kubwa.

Unajua haya yote yanatokana na nini? Sababu zote hizi tunaendelea kujifunza kwenye uchambuzi wa kitabu RICH DAD POOR DAD. Hapa tutazungumzia machache kwa ufupi na kama utapenda kujifunza zaidi nitakuambia ufanye nini mwishoni.

1. Elimu ya fedha haitolewi shuleni. Mfumo wa elimu hautoi elimu ya fedha na hivyo watu wengi licha ya kuwa na elimu kubwa wanajikuta kwenye matatizo ya kifedha.

2. Ukosefu wa elimu ya fedha umekufanya uingie kwenye mbio za panya. Asilimia kubwa ya watu wako kwenye mbio za panya, hata wewe kuna uwezekano mkubwa upo kwenye mbiuo za panya. Unajua mbio za panya ni nini? Unaamka asubui, unakwenda kazini, unafanya kazi, unarudi nyumbani, unasubiri mshahara na ukishapokea mshahara unakwenda kulipa madeni. Mwezi mwingine unarudia tena hivyo hivyo mpaka kustaafu.

Binadamu wote tunaathiriwa na hisia mbili kwenye fedha;

3. Hisia ya kwanza ni hofu. Unapokuwa huna fedha unakuwa na hofu kwambamaisha yakakuwa magumu, utrashindwa kula, kulala na hata kupata matumizi mengine ya msingi. Hofu hii inakusukuma ufanye kazi kwa bidii sana.

4. Hisia ya pili ni tamaa. Baada ya kufanya kazi na kupata fedha, tamaa ya kuanza kuzitumia inakujia. Unajikuta unatumia fedha hizo kununua vitu ambavyo havina faida kubwa kwako. Unapokuwa na fedha unaona nguo nzuri, gari zuri, simu nzuri na hata samani nzuri amabazo unatamani kuzinunua. Na jinsi unavyopata kipato kikubwa ndivyo unavyozidi kuwa na tamaa ya kutumia zaidi.

Hisia hizi mbili zimewafanya watu wengi kuwa watumwa wa fedha maisha yao yote.

5. Tatizo lako sio kipato kidogo bali mtazamo wako kuhusu fedha. Waajiriwa wengi wanaa mini kwamba sababu kubwa ya wao kuwa na matatizo ya fedha ni kwa vile wanalipwa fedha kidogo. Lakini hata inapotokea mshahara ukaongezwa bado matatizo hayo hayaishi na wakati mwingine yanakuwa mengi zaidi. Tatizo lako sio mshahara kidogo, sio mwajiri wako, sio serikali na wala sio uchumu. Tatizo ni wewe kukosa elimu ya fedha.

6. Tofauti kati ya masikini na tajiri sio kipato wanachopata bali matumizi ya kipato wanachopata. Masikini akipata fedha anapeleka yote kwenye matumizi na kununua mali zisizozalisha. Tajiri aki[ata fedha ananunua mali zinazozalisha na hivyo mali hizo kuwazalishia zaidi.

7. Jua tofauti kati ya mali zinazozalisha(ASSETS) na mali zisizozalisha(LIABILITIES). ASSETS ni kitu ambacho kinaingiza fedha mfukoni mwako. LIABILITY ni kitu ambacho kinatoa fedha kwenye mfuko wako.

8. Nyumba yako sio ASSET. Ndio, nyumba unayoishi sio asset kwa sababu haikuingizii fedha moja kwa moja na pia inakuingizia gharama ambazo inabidi ulipe. Kwa mfano unapokuwa na nyumba kubwa unakuwa na bili kubwa ya umeme, bili kubwa ya maji, unahitaji kuweka marembo mengi, unahitaji kuweka samani nyingi na pia unailipia kodi ya majengo. Kwa gharama zote hizi nyumba haiwezi kuwa ASSET. Najua utapinga hili kwa sababu benki itakuambua nyumba yako ni asset na ni kweli ni asset ila ni kwa benk na sio kwako wewe.

Haya ni machache sana kati ya mengi ambayo tunaendelea kujifunza kwenye uchambuzi huu wa vitabu. Kama unataka kujifunza zaidi na pia unataka kujua unawezaje kutatua matatizo hayo hapo juu jiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Kujua jinsi ya KUJIUNGA NA KISIMA CHA MAARIFA 

Jiunge leo ili usipitwe na darasa hili muhimu litakalokusaidia kuweza kufikia uhuru wa kifedha.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia uhuru wa kifedha.

TUKO PAMOJA.

kitabu kava tangazo