Hofu ni hali ya kuwa na wasiwasi wa kitu fulani kibaya kutokea lakini kitu hicho huwa bado hakija tokea.

Kama binadamu kila mmoja hupatwa na woga kwa nyakati tofauti. Woga huu hugusa maeneo mbalimbali katika maisha ya kila siku yaweza kuwa kazini, katika mahusiano, katika matembezi,kwenye ndoa. N.k.

Kila binadamu anahofu yake.

SOMA; Orodha Mpya Ya Mabilionea; Mambo Kumi Ya Kuzingati Ili Na Wewe Uweze Kuingia Kwenye Orodha Hii Siku Za Baadae.

Hofu inaweza kuwa mbaya au hofu nzuri kutegemeana na hofu uliyonayo. Mfano hofu ya kupoteza pesa baada ya kusikia kuna mahali ukihifadhi pesa kwa wiki moja utapewa mara tatu zaidi. Hii ni hofu nzuri. Inawezekana ukajiuliza kitu kama hiki kinaukweli gani, mbona hakuna utarartibu kama huu hapa ulimwenguni wa kuweka pesa na kukaa tu halafu baada ya wiki ukapewa maratatu ya pesa hizo.

Waswahili wanasema woga wako ndio umasikini wako. Kuna baadhi ya watu huogopa kufanya jambo lolote kwa kuwa na fikra hasi za baadae. Ni vizuri kuchukua tahadhari kwa kila jambo unalotaka kulifanya na sio kuogopa tuu. Kumbuka kuwa uoga ni wasiwasi wa kitu kuleta matokeo mabaya, sio kwamba jambo baya limeshatokea tayari.

NINI CHANZO CHA HOFU/WOGA

Chanzo cha hofu au woga ni hisia za ndani ambazo zimejengeka katika jamii yetu kutoka kwa wazazi wetu na watu wa karibu wanaotuzunguka au watu ambao wamepata matatizo fulani baada ya kufanya jambo fulani, hivyo kutufanya nasi kuwa na woga.. Mara nyingi tumekua tukiambiwa kuwa usiposoma huwezi kufanikiwa, huwezi kuwa kiongozi mkubwa,ukiwa tajiri utarogwa, matajiri wote ni wanyonyaji,huwezi kupata kazi kama huna mtu wa juu wa kukuunganishia,ndoa ni mbaya sana bora usioe au usiolewe na maneno mengine mengi ya kuogopesha. Maneno haya na mengine mengi yamejenga hofu za kila namna kwenye kila eneo la maisha yetu na hivyo kuyaona maisha ni magumu na mabaya kila tukikumbuka hofu hizo.

SOMA; Hizi ndio Hofu mbili ulizozaliwa nazo, nyingine ni uongo.

NAMNA YA KUONDOKANA NA HOFU NA KUISHI KWA FURAHA

Kuondokana na HOFU/WOGA huu sio jambo rahisi sana lakini habari njema ni kwamba kama ukiamua kwa dhati inawezekana kuishi bila hofu na woga utakaokufanya usitimize ndoto zako.

Kwanini sio rahisi, tumezungukwa na watu ambao wanatuogopesha hata ukijaribu kuondoa woga sauti zote zinazokuzunguka zitakuambia maneno ya kuogopesha. Inahitaji ufahamu kuwa wewe mwenyewe ndiye kiongozi wa maisha yako na unaweza kuamua kuachana na hofu hizo bila kusubiri mtu mwingine yeyote kukusaidia kuondo hofu hizo. Kwakua asilimia kubwa ya watu wanaotuzunguka wanahofu na woga. Wamekua katika mazingira hayo na woga na hofu imekuwa sehemu ya maisha yao.

SOMA; UKURASA WA 17; Hofu, Matumizi Mabaya Ya Ubunifu Wako.

UFANYE NINI SASA

Vile unavyoamini toka ndani ndivyo inavyokuwa katika ulimwengu wa nje. Ukiwa na hofu kuwa kila tajiri ni mdhulumaji basi utawachukia matajiri wote na wewe pia utaishia kuwa masikini na kuridhika na hali uliyonayo lakini bado hautakuwa na furaha kwasababu huwezi kukidhi mahitaji yako ya kila siku,

Kaa mahali penye utulivu na ujiulize ni hofu gani inayotawala maisha yako na inayozuia maendeleo yako?

Ni hofu gani uliyonayo? Andika hofu hiyo katika karatasi.

Fikiria kama kuendelea kuwa na hofu hiyo kutaleta mabadiliko yoyote mazuri katika maisha yako,

Jiulize kama unataka kuendelea kushikilia hofu hiyo mwisho wake utakuwa mzuri?

Je kuna namna unavyoweza kuchukua tahadhari kwa kuondoa hofu na kufanya jambo ambalo unahitaji kulifanya na unaona ni muhimu na litakamilisha furaha ya moyo wako. Andika namna utavyofikiri ni njia nzuri ya kuondoa hofu hiyo na kupata nguvu ya kutimiza ndoto yako.

SOMA; SIRI YA 24 YA MAFANIKIO; Fanya Licha Ya Kuwa Na Hofu.

Acha kabisa kufikiria hofu hiyo badala yake fikiria matokeo ya mwisho mazuri ya jambo utakalolifanya na endelea kuwa makini ukichukua tahadhari.

Fanya hivi kwa kila hofu inayokuzuia kuzifia ndoto zako. Baada ya muda utahisi umefunguka na unaishi kwa amani na furaha na mambo mazuri yanaendelea kutokea katika maisha yako.

Maisha ya furaha na amani yanawezekana. Chukua hatua sasa.

Mwandishi: Esther Ngulwa.

Mawasiliano: estherngulwa87@gmail.com

0767 900 110/ 0714 900 110/ 0784 576 131