Katika watu wote waliofikia mafanikio makubwa, kuna kitu kimoja ambacho kinapatikana kwa kila mmoja. Kitu hicho ni imani imara kwamba wanaweza kufikia mafanikio makubwa sana kwenye kile wanachofanya.
Hijalishi ni kitu gani umechagua kufanya au kupata, unaweza kufanya au kupata chochote unachotaka. Lakini ni lazima ufanye mambo haya matatu;
1. Ni lazima uamue ni kitu gani hasa unachotaka kwenye maisha yako na ufanye kitu hiko kuwa lengo lako la maisha.
2. Ni lazima uamini kwa moyo mmoja na bila wasiwasi wowote kwamba unaweza kupata kile unachotaka.
3. Ni lazima uwe tayari kulipa gharama inayohitajika kulipa ili uweze kupata kile unachotaka. Kila kitu kina gharama ya kulipia, inaweza kuwa muda, fedha, kuacha tabia zinazokuzuia kufanikiwa na mengineyo.
Muhimu zaidi ni lazima utumie njia za mafanikio zilizodhibitishwa ili kuweza kufikia mafanikio unayotarajia. Njia hizo utaendelea kujifunza katika siku hizi 30.
Kama mafanikio ni rahisi hivi kufikiwa kwa nini watu wengi hawajafanikiwa?
Watu wengi hawajafanikiwa kwa sababu hawajui ni jinsi gani wanaweza kufikia mafanikio makubwa. Hawatumii njia za mafanikio zilizodhibitishwa. Wanatumia njia za kushindwa ambazo zinawahakikishia kushindwa. Kwa mfano watu wengi wanajua ni kitu gani wanataka ila hawaamini bila ya shaka kwamba wanaweza kupata kitu hiko. Mawazo yao yanakuwa na mashaka makubwa kwamba watashindwa kupata kile wanachotaka na hivyo kushindwa kukipata.
Kama ukiamini bila ya kuwa na shaka kwamba utafanikiwa, hakika utafanikiwa. Hata kama sasa bado huna mafanikio au huna elimu ya kukufikisha kwenye mafanikio hayo utavipata vyote hivyo kama kweli ukiamini unaweza.
Unawezaje kujijengea imani hii ya kwamba unaweza kufanikiwa?
Kitu kikubwa ambacho mpaka sasa kinakurudisha nyuma ni kukosa imani kwako mwenyewe na kushindwa kuwa na imani imara kama unaweza kufanikiwa. Hivyo kazi ya kwanza unayotakiwa kufanya ni kuanza kujitambua wewe mwenyewe binafsi.
Onekana kama mtu mwenye mafanikio, fikiri kama mtu mwenye mafanikio, tenda kama mtu mwenye mafanikio, Amini bila ya shaka kwamba utafanikiwa na hakika UTAFANIKIWA.
Unapokuwa na imani imara kwamba utafanikiwa anza kuweka mipango yako ukiwa na uhakika kwamba ni lazima utaifikia. Fikiria ukiwa na uhakika, kuwa na mtizamo wa kuwa na uhakika na pia tenda ukiwa na uhakika kwamba unakwenda kupata kile unachotaka kupata.
Nakutakia kila la kheri katika safari ya kufikia mafanikio makubwa. Karibu kwenye FORUM YA SIKU 30 ZA MAFANIKIO ili tuweze kuendelea kujadiliana.(bonyeza hayo maandishi kuingia kwenye mjadala)
TUKO PAMOJA.