KITABU; As You Think(Jinsi Unavyofikiri Ndivyo Ulivyo)

Karibu tena msomaji wa AMKA MTANZANIA katika utaratibu wa kujisomea vitabu. Katika utaratibu huu kila mwezi unatumiwa kitabu kimoja ambacho kama ukikisoma kinakuwa na msaada mkubwa kwako.

Mwezi huu nakushirikisha kitabu AS YOU THINK kilichotokana na kitabu AS A MAN THINKETH ambacho kiliandikwa na James Allen.

Kitabu hiki AS YOU THINK kimechambua vizuri sana mawazo unayoweka kichwani kwako na mambo yanayotokea kwenye maisha yako.

Yote yanayotokea kwenye maisha yako sio kwa bahati mbaya au yanatokea tu, bali yanatokana na mawazo ambayo umewahi kuwa nayo kwenye kichwa chako.

asyouthink

Kitabu hiki kimegawanyika kwenye sehemu saba;

1. Mawazo na tabia. Uko hivyo ulivyo kutokana na mawazo yaliyopo ndani yako, tabia zako na zao la mawazo yako.

2. Madhara ya mawazo kwenye matukio. Unapata kile ambacho unawaza. Akili ya binadamu ni sawa na shamba lenye rutuba, likipandwa mazao mazuri linazaa mazao mazuri na lisipopandwa magugu huota. Hivyo ukiwa na mawazo mazuri utapata matokeo mazuri, usipokuwa na mawazo mazuri kila wazo linaingia na kuleta madhara.

3. Madhara ya mawazo kwenye mwili. Mwili wako ni kijakazi wa mawazo yako. Mwili hupokea kile ambacho akili inawaza, ukiwaza kuwa na afya unakuwa nayo tele, ukiwaza kuwa na magonjwa yatakuandama.

4. Mawazo na malengo. Bila mawazo kuelekezwa kwenye lengo fulani hakuna kitakachoweza kufikiwa. Kama mawazo yako utayaelekeza kwenye lengo moja unalotaka kufikia utalifikia.

5. Mawazo na mafanikio. Yote ambayo tunafanikiwa kuyapata na hata yale tunayoshindwa kuyapata yote yanatokana na mawazo ambayo yako ndani yetu. Kama unafikiri unaweza ni kweli unaweza na kama unafikiri huwezi ni kweli huwezi.

6. Maono na mategemeo. Dunia inaendeshwa na wale ambao wana maono na mategemeo makubwa. Na yote haya hutokana na mawazo mazuri anayokuwa nayo mtu.

7. Utulivu. Utulivu wa akili ndio chanzo cha busara, unaweza kuwa na utulivu wa akili pale ambapo unaweza kujidhibiti mwenyewe.

Download kitabu hiki na ukisome na kukirudia tena na tena kukisoma na utaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako kama utatumia yale ambayo unajifunza.

Kitabu hiki ni kifupi sana(kina kurasa 28 tu) hivyo unaweza kukisoma kwa saa moja tu na kikawa kimeisha.

Kupata kitabu hiki bonyeza jina hili la kitabu; AS YOU THINK.

Kupata vitabu vya zamani kama hukuvipata bonyeza maandishi haya na utakuta makala zilizoelezea vitabu hivyo na jinsi ya kuvipata.

Pia karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA ambapo tunaendelea na uchambuzi wa vitabu na sasa tunachambua kitabu RICH DAD POOR DAD.

Usisahau kupata application ya simu yako ambayo itakuwezesha kupata habari moja kwa moja kwenye smartphone au tablet yako. Kupata APP hiyo bonyeza maandishi haya na ufuate maelekezo.

Nakutakia kila la kheri katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.

TUKO PAMOJA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: