Ni muhimu kukumbuka kwamba watu wote waliofikia mafanikio makubwa walikuwa wamejitoa kweli kwa ajili ya kufikia mafanikio. Waliamini bila kuyumbishwa kwamba dunia imejaa utajiri na kinachohitajika ni wewe kuwa na ufunguo wa siri wa kufungua milango itakayokuletea mafanikio.

Leo tutajifunza sheria za asili ambazo zinaweza kukuletea mafanikio na utajiri mkubwa. Ni sheria za asili kwa sababu zinafanya kazi mahali popote na kwa mtu yeyote.

1. Sheria ya Matendo.

Hii ni sheria muhimu sana ya kufuata. Mafanikio yanatokana na matendo unayofanya, ukifanya kidogo unapata kidogo, ukifanya sana unapata makubwa. Hata uwe na mawazo mazuri kiasi gani huwezi kufikia mafanikio kama hutayafanyia kazi mawazo yako.

Kutengeneza mtiririko mzuri wa mafanikio. Kuwa na kitabu chako cha mafanikio ambapo kila siku utakuwa unaandika mawazo ya kukuwezesha kufikia mafanikio. Kisha fanyia kazi mawazo hayo. Ni lazima uanze kuyafanyia kazi mawazo yako sasa, usisubiri muda muafaka au kupata mtaji zaidi. Anza kutenda na utapata njia zaidi za kuboresha.

2. Sheria ya uadilifu.

Msingi mkuu wa kufikia mafanikio ni uadilifu. Hakuna mafanikio yanaweza kufikiwa bila ya uadilifu, na hata ikitokea hayadumu kwa muda mrefu. Kuwa muaminifu kwako na kwa wengine pia na utapata fursa nyingi sana za kufikia mafanikio. Kuna sheria chache za kujijengea uadilifu;

a/. Wafanyie wengine kile ambacho ungependa wao wakufanyie.

b/. Kuwa muaminifu kwako na kwa wengine pia. Usidanganye, ususengenye, na wala usisaliti.

c/. Usimuibie mwingine mali au muda wake. Timiza ahadi zako.

d/. Tengeneza kila siku yako katima misingi ya uaminifu na hutakuwa na haja ya kuogopa kushindwa kwenye maisha.

3. Sheria ya kutoa na kupokea.

Katika kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla unatoa ndipo unapokea. Ni lazima utoe ndipo uweze kupokea, unatoa thamani kwenye biashara yako unapatafaida. Unatoa muda na ujuzi wako kwenye kazi unapata mshahara na hata kupata fedha inabidi utoe fedha. Matatizo makubwa kwenye maisha yanaanzia pale watu wanapotaka kupata zaidi ya wanachotoa. Au wengine hawatoi kabisa ila wanataka kupata.

Hivyo hakikisha unatoa kile ambacho kinalingana na unachotarajia kupokea ili uweze kufikia mafanikio makubwa.

4. Sheria ya ubunifu wa taswira.

Hii ni sheria muhimu sana. Watu waliofanikiwa waliweza kupata picha ya mafanikio yao. Na pisha hii ndio iliwawezesha kufikia mafanikio yao bila ya kukata tamaa.

Kama tulivyoona kwenye makala ya SIKU YA 20, pata muda wa kutengeneza picha ya mafanikio unayotaka na kila siku ipitie picha hiyo kwenye mawazo yako. Kwa kufanya hivi utakuwa unajisogeza karibu na mafanikio unayotaka kufikia.

5. Sheria ya akili yako ya ndani.

Una akili tatu, akili ya kufikiri(conscious mind), akili isiyofikiri(subconscious mind) na akili ya juu(superconscious mind). Conscious mind ndio akili unayotumia kufanya maamuzi ya kila siku. Subconscious mind haifanyi maamuzi ila inapokea taarifa zote ambazo unaingiza kwenye mawazo yako. Na inakutengenezea mazingira ya taarifa unazoingiza. Ndio maana wanaowaza kushindwa kila siku wanashindwa na wanaowaza kufanikiwa kila siku wanafanikiwa.

Tumia uwezo huu mkubwa wa subconscious mind yako na weka mawazo ya mafanikio muda wote na utafikia mafanikio makubwa.

6. Sheria ya tajahudi/taamuli(meditation).

Hii ni sheria ambayo imekuwa inatumiwa na watu wengi waliofikia mafanikio makubwa. Kupitia meditation mtu anaweza kufikia uwezo wake mkubwa na kuweza kutumia mawazo yake mazuri. Meditation inamfanya mtu kuacha mawazo yanayosumbua na kukaa na wazo moja ambalo linamwezesha kufikia mafanikio makubwa.

Nitakuja kuandika zaidi kuhusu meditation, ila kama hujui kabisa ni nini soma makala hii; jinsi ya kufanya meditation na faida zake.

Nakutakia kila la kheri katika safari ya kufikia mafanikio makubwa. Karibu kwenye FORUM YA SIKU 30 ZA MAFANIKIO ili tuweze kuendelea kujadiliana.(bonyeza hayo maandishi kuingia kwenye mjadala)

TUKO PAMOJA.