Zimebaki Siku 100 Mwaka 2014 Uishe, Fanya Kitu Hiki Kimoja Unufaike Na Siku Hizi 100.

Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, naamini uko vizuri na unaendelea na safari ya kuboresha maisha yako. Kufikia leo tarehe 22/09/2014 zimebaki siku 100 tu mwaka huu uishe. Yaani tayari tumeshakata siku 260 za mwaka huu. Swali ni je umefanya nini kwenye siku hizi 260?

Unakumbuka malengo na mipango uliyojiwekea mwaka huu 2014? Ni vingapi umetimiza? Unakumbuka malengo yako ya kila mwaka kwamba utaanzisha au kukuza biashara yako ili uondokane na matatizo ya kifedha? Umefikia wapi kwa mipango hiyo?

milliondollarhabits_detail5

Leo kaa chini na ujiulize maswali hayo na mengine mengi sana kuhusu maisha yako, ulikotoka, uliko na unakoelekea. Angalia jinsi ambavyo kila mwaka umekuwa unakuja na kupita huku wewe ukibaki vile vile. Angalia jinsi ambavyo maisha yanazidi kuwa magumu kila siku huku ukiona hakuna unachoweza kufanya. Angalia jinsi ambavyo kazi unayofanya umekuwa huipendi na inakuwa chanzo cha msongo wa mawazo kwako.

Angalia yote haya na ujiulize je hayo ndio maisha unayotaka kuendelea kuwa nayo miaka mitano, kumi na hata ishirini ijayo? Je unataka kufa na miaka 35 na kuzikwa na miaka 65?

Naamini unahitaji maisha bora zaidi, unahitaji maisha yenye maana kwako na wanaokuzunguka na unahitaji kuwa na uhuru wa kifedha, na kazi ambayo unafurahia kuifanya. Sasa yote haya yanawezekana na leo nitakupa kitu kimoja cha kukuwezesha kufanya.

Angalia, uko hapo ulipo kutokana na wewe mwenyewe. Ndio unaishi maisha unayoishi na kazi au biashara unayofanya kutokana na baadhi ya maamuzi uliyowahi kufanya kipindi cha nyuma na unayoendelea kufanya kila siku. Na maamuzi haya yanatokana na tabia ulizozitengeneza tokea unazaliwa na kukua mpaka sasa. Na tabia hizi zinatokana na mawazo unayoingiza kwenye kichwa chako.

Kwa kifupi nasema hivi; umekuwa na mawazo ambayo yamezalisha tabia na tabia hizi zimekufikisha hapo ulipo sasa. Kwa hiyo ili kuondoka hapo unahitaji kubadili mawazo unayoweka kwenye kichwa chako, kubadili tabia na hatimaye kuweza kufanya maamuzi sahihi yatakayokuletea mafanikio.

Ndio maana leo nataka nikushirikishe kitu kimoja utakachokifanya kwenye siku hizi 100 zilizobakia na uufanye mwaka 2014 kuwa mwaka wa kumbu kumbu kwenye maisha yako.

Kitu hiki nachokuambia ufanye sio kigeni kwako, nimekuwa nikikishauri kila mara ila kwa sababu moja au nyingine umekuwa hukiweki maanani. Sasa mambo yanazidi kuwa magumu kwako hivyo huna budi bali kukiweka maanani sasa.

Kitu ninachokushauri na hata kukuomba sana ukifanye ni kubadili mawazo/fikra zako, kubadili tabia zako na hatimaye kuweza kufanya maamuzi bora na sahihi kwako na kwa wengine pia. Na ili kuweza kufanya hivyo nimekuandalia kitu kizuri sana kitakachoweza kukusaidia kufanya hivyo.

Nimekuandalia kitabu kizuri ambacho kitaweza kufanya mambo hayo matatu, kukubadilisha mawazo, kukufundisha tabia za kuchukua na kukuwezesha kufanya maamuzi mazuri. Ninachokuomba ni wewe uanze kusoma kitabu hiko leo, kwa nusu saa tu utakayoitenga na kuanzia kesho uamke nusu saa kabla ya muda uliozoea kuamka na uendelee kusoma kitabu hiki. Fanya hivi kila siku kwa siku hizi 100 na kama maisha yako yataendelea kuwa magumu nitafute nikulipe nusu saa zote ulizopoteza kwa siku 100. Soma mambo unayopata kwenye kitabu hiki na anza kuyatumia kwenye maisha yako, kazi na hata biashara zako.

Kitabu ninachokushirikisha kinaitwa Million dollar habits kilichoandikwa na Brian Tracy. Ni kitabu ambacho kwa kukisoma utaweza kubadili tabia zako na kujenga tabia zitakazokuletea mafanikio, furaha na afya njema. Kitabu hiki kimeandikwa kwa mfumo ambao unaweza kukisoma vizuri sana kwani kina vipengele vidogo vidogo.

Kwa wale ambao tayari ni wanachama wa AMKA MTANZANIA bonyeza maandishi haya ya kitabu Million dollar habits na utaweza kukipakua na kuanza kukisoma(kama unasoma kwenye blog nenda kwenye email yako).

Kama bado hujawa mwanachama bonyeza hapa na uweke email yako na ujiunge kisha utatumiwa email yenye kitabu hiki na vingine vitatu.

Umeishi miaka mingi sasa bila ya kufanya jambo lolote la kuweza kukubadili kabisa wewe. Naomba basi utumie siku hizi 100 tu kusoma na kutumia hayo unayoyasoma kwenye kitabu hiko na kama ukiona hayana maana yoyte kwenye maisha yako basi rudi kwenye maisha yako ya kawaida.

Nakutakia kila la kheri kwenye safari ya kuboresha maisha yako. Napenda sana maisha yako yawe bora kwa sababu najua uwezo wa kuyaboresha unao. Na ndio maana nakusisitiza na kukuomba uchukua hatua hii ndogo kuanza kubadili maisha yako.

TUKO PAMOJA, TUTAKUTANA KILELENI.

PS.

Kwa wale ambao ni wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ambao waliomba kuwepo kwenye kujenga tabia ya kuamka asubuhi na kujisomea kitabu tunatumia kitabu hiki na zoezi limeanza leo. Kama na wewe ungependa kupata nafasi hii, bonyeza maandishi haya kupata utaratibu wa kujiunga na kisima cha maarifa na ujiunge kwa GOLD MEMBER ili kuweza kuzitumia siku hizi 100 vizuri.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s