Vitu vyote vina mizizi yake kwenye imani. Kila kitu tunachofanya kwenye maisha kinaanzia na imani.
Tunaamini kwamba chakula tunachokula kitaenda kujenga miili yetu na hivyo kutupatia afya bora japokuwa hatujui inatokeaje.
Tunaamini kwamba hewa tunayovuta ina mchanganyiko mzuri ambao unahitajika kwenye miili yetu kwa ajili ya kutupatia nguvu.
Tunaamini kwamba jua litachomoza kila subuhi, dunia itaendelea kuzunguka na nyota zitaendelea kuwepo angani.
Imani ndio kitu kimoja muhimu sana ambacho kimetuwezesha mapaka sasa kuendelea kuwepo duniani.
Imani na akili ya ndani.
Kama tulivyoona kwenye makala zilizopita, akili zetu zina sehemu tatu, akili inayofikiri(conscious mind), akili isiyofikiri(subconscious mind) na akili inayoongoza zote kwa imani(superconscious mind).
Subconscious mind inapokea kila wazo ambalo unaingiza kwenye akili yako. Akili hii haina uwezo wa kujua kama hili ni jema au baya. Bali hupokea kila wazo na kuanza kulifanyia kazi. Kwa kuwa mtu hupata mawazo mengi sana kwa siku, subconscious mind yake haiwezi kuyafanyia kazi mawazo yote hayo. Bali hufanyia kazi mawazo yale ambayo yanajirudia kila mara. Hii ndio sababu wale wanaofikiri watapata mafanikio, huyapata kweli na wale wanaofikiri kushindwa kila wakati huishia kushindwa.
Kama ukiwa na mawazo ya mafanikio ambayo unayarudia kila siku na kuamini kwamba hiki ndio kitakachotokea kwneye maisha yako basi subconscious mind yako itakuweka kwenye mazingira ya kufikia mafanikio hayo.
Mawazo na imani huumba.
Kama tulivyoona hapo juu kuhusu subconscious mind mawazo yoyote ambayo yamewekewa imani kali hutokea. Kama unafikiri kwamba wewe unaumwa na ukaamini hivyo bila ya kuyumbishwa basi unapata ugonjwa. Kama unafikiri kwamba wewe utafanikiwa na kuamini hivyo bila ya kuyumbishwa ni lazima utafikia mafanikio. Hii ni kwa sababu subconscious mind yako inakutengenezea mazingira ya kufikia kile ambacho kimetawala kwenye subconscious mind yako.
Imani na uthibitisho.
Subconscious mind yako inataka uthibitisho wa kitu ili iweze kukifanyia kitu hicho kazi. Na njia moja ya kuthibitisha kitu kwenye subconscious mind yako ni kurudia kukifikiaria au kukisema kitu hiko kama vile tayari umeshakipata. Kama utafikiria na kujiambia kwamba tayari una mafanikio, tayari unafedha, tayari una afya bora yote haya yatajengwa kwenye imani na utaweza kuyafikia.
Mara zote kumbuka; Subconscious mind yako inakutengenezea kile ambacho unakiamini.
Maamuzi ni kukubali.
Maamuzi yoyote tunayofanya kwenye maisha kwa kujua au kutokujua ni kukubaliana na hali ilivyo. Kwa mfano tuseme umeamua kufanya biashara yako na umeshajiwekea imani kwamba utafanikiwa kwneye biashara hiyo. Umekwenda kununua bidhaa na kuziweka kwenye eneo lako la biashara. Siku zinapita ila hakuna mnunuzi yoyote anayekuja kununua biadhaa zako. Katika hali hii nini kinatokea? Unaanza kufikiria umefanya makosa kuingia kwenye biashara yako, kwenye mawazo yako unaanza kupata picha kwamba unakwenda kupata hasara kubwa. Katika wakati huu unafikiria kushindwa kwa muda mrefu na hivyo subconscious mind yako inajua hiko ndio unachokitana na kinatokea kweli.
Ila usipokubaliana na mawazo haya na ukaendelea kufikiria ni njia gani unaweza kuzitumia ili kuondoka kwenye hali hiyo subconscious mind yako itakutengenezea njia nyingi sana na hivyo utaweza kufikia mafanikio makubwa.
Kumbuka ni muhimu kufikiria mafanikio ili ufanikiwe. Hakuna anayefirikia kushindwa akafanikiwa.
Mawazo chanya.
Moja ya vitu vinavyowarudisha watu wengi nyuma ni mawazo hasi juu yao wenyewe. Ni muhimu kuwa na mawazo chanya ili kuweza kufikia mafanikio makubwa. Sehemu kubwa ya maisha yako umekuwa ukiendeshwa na mawazo hasi. Ili kuondoa mawazo haya hasi utakwenda kufanya zoezi hili la siku 30.
Kwa siku 30 zijazo jitahidi kila siku kufikiria mawazo chanya tu, pale wazo hasi linapokuja kwenye mawazo yako achana nayo haraka sana na endelea kufikiria mawazo chanya juu yako na kazi au biashara unayofanya.
Ni kupitia mawazo haya chanya ndio utaweza kuvunja tabia mbaya ulizonazo na kutengeneza tabia nzuri zitakazokuletea mafanikio makubwa.
Hivi ndivyo imani ilivyo muhimu kwako kufikia mafanikio makubwa. Jenga na imarisha imani yako kwamba unaweza kupata chochote unachotaka na hakika utakipata.
Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
TUKO PAMOJA.