Katika jamii yoyote ile kuna madaraja tofauti kimapato na hata kifikra.
Leo tutajadili kuhusu madaraja ya kifikra, maana madaraja haya ndio yanazalisha vipato tofauti kwenye jamii zetu.
Aina za madaraja ya kifikra
1. Daraja la masikini(poverty class)
Hili ni daraja la wale ambao wanafikiria watakula nini na baada ya kula wanafikira mlo ujao watakula nini tena. Hawana fikra kubwa na malengo makubwa ya baadae, wana matatizo mengi yanayowasonga na hivyo hawawezi kufikiri mbali.
2. Daraja la wafanyakazi(working class)
Hili ni daraja la watu wanaofanya kazi kwa nguvu sana ila bado hawaoni mafanikio makubwa. Watu hawa wanaweza kulalamika wanafanya kazi sana lakini wananyonywa au hawajui fedha zinaenda wapi.
3. Daraja la kati (middle class)
Hili ni daraja ambapo mtu anaweza kupata mahitaji yake muhimu, anaweza kuonekana tajiri ila kama kazi anayofanya ikiisha leo maisha yake yanabadilika na kuwa ya hali ya chini sana. Hawa ni watu ambao wana kipato kikubwa ila pia wana matumizi makubwa na wanapenda kuonekana wana vitu vya thamani.
4. Daraja la juu(upper class)
Hili ni daraja ambapo mtu anakuwa na kipato kizuri, maisha mazuri ila pia amejipanga kwa siku za mbeleni. Hivyo hata ikitokea kazi imekwisha bado anaweza kuendesha maisha yake kwa siku atakazoendelea kuishi.
5. Daraja la kimataifa(world class)
Hili ni daraja la juu kabisa ambapo mtu aliyepo kwenye daraja hili ana uelewa wa juu sana kwa kile anachofanya na ana maisha mazuri na hata asipofanya kazi ana fedha za kumtosha kutumia yeye na hata watoto wake na wajukuu zake.
Baada ya kujua tofauti hizi tano za madaraja katika jamii zetu nina hakika kila mmoja wetu anachagua kuwa world class, kwa sababu unaamini unaweza kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa. Pia kwa nchi zetu hizi bado world class ni wachache sana hivyo inatufanya sisi tunaopanga kufikia world class iwe njia rahisi kwetu.
Ili kuondoka kwenye middle class ambapo upo sasa na kwenda kwenye world class kuna mambo mengi ya kuanza kubadili. Hapa tutajadili tofauti kati ya middle class na world class ili ujue ni vitu gani vya kuacha kufanya na ni vitu gani vya kuanz akufanya ili kuweza kuelekea kwenye mafanikio makubwa.
Tofauti kati ya world class na middle class.
1. Middle class wanashindana wakati world class wanatengeneza vitu vipya.
2. Middle class wanaepuka hatari wakati world class wanadhibiti hatari.
3. Middle class wanaishi kwenye ndoto, world class wanaishi kwenye uhalisia.
4. Middle class wanapenda kuridhika, world class wameridhika na kutoridhika.
5. Middle class wana akili ya bahati na sibu, world class wana akili ya utajiri usio na kikomo.
6. Middle class wanatafuta usalama, world class hawaamini kama kuna usalama.
7. Middle class wanaacha kukua ili kuwa salama, world class wanaacha usalama ili kukua.
8. Middle class wanafanya kutokana na hofu na uhaba, world class wanafanya kutokana na mapenzi na wingi.
9. Middle class wanaweka mkazo kwenye kuwa na vitu, world class wanaweka mkazo kwenye kuwa tofauti.
10. Middle class wanajiona kama waonewa, world class wanajiona kama wao ndio wana majukumu na maisha yao.
11. Middle class wamevurugwa, world class wanashukuru.
12. Middle class wana ndoto ndogo, world class wana ndoto kubwa.
13. Middle class wanaongozwa na ufahari, world class wanaongozwa na imani.
14. Middle class wanafikiria matatizo, world class wanafikiria suluhisho.
15. Middle class wanafikiri wanajua vya kutosha, World class wana kiu ya kujifunza zaidi.
16. Middle class wanachagua hofu, world class wanachagua kukua.
17. Middle class wanapenda kujisifia, world class ni wanyenyekevu.
18. Middle class wanauza muda ili kupata fedha, world class wanauza mawazo kupata fedha.
19. Middle class wanatafuta utajiri wa muda mfupi, world class wanatafuta utajiri wa muda mrefu, uhuru wa kifedha.
20. Middle class wanaamini maono yao baada ya kuyaona, world class wanaona maono yao baada ya kuyaamini.
21. Middle class wanaongea lugha ya woga, world class wanaongea lugha ya upendo.
Yafanie mambo hayo 22 kazi na utakuwa na uhakika wa kufikia viwango vya world class kwenye jambo lolote unalofanya.
Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
TUPO PAMOJA.