Tunaendelea na sehemu ya pili ya uchambuzi wa mjadala ulikuwa unaendelea kuhusu bahati.

Arkad na mkusanyiko ule wa atu waliendelea kujadili ikiwa kweli kuna bahati au kuna miungu ambayo inatoa bahati. Arkad aliendelea kusisitiza kwamba faida yoyote inatokana na kujituma na kufanya kazi na sio bahati tu. Watu wengi waliendelea kusisitiza kwamba kuna bahati na wakasema kuna wakati mtu anakuwa bahati inaelekea kwake ila inapotea.

Katika kueleza hilo, mfanya biashara mmoja aliamka na kusema kwa kutumia mfano kwamba wakati akiwa kijana baba yake alimfuata na kumwambia kwamba mtoto wa rafiki yake anatafuta watu wa kufanya nae uwekezaji. Alimwambia kwamba kijana huyo alikuwa amepata eneo lililopo kwenye mlima ambapo maji hayafiki na hivyo alitaka mtu wa kushiriakiana nae ili waweze kufikisha maji kwenye eneo lile. Na baada ya kufikisha maji wangegawa eneo lile katika sehemu ndogo ndogo na kuuza kwa watu wanaohitaji maeneo. Aliendelea kusema baba yake alimsisitiza sana kwamba huu ni uwekezaji mzuri sana na kama ingekuwa enzi za ujana wake angeufanya. Alimwambia yeye alifanya makosa mengi sana wakati wa ujana wake na hivyo kukosa fursa nyingi. Alimshauri asisite site na achukue hatua mapema maana uwekezaji huo utawalipa sana. Bwana huyu hakuchukua hatua na badala yake alitumia fedha zake kununua urembo wake na wa mke wake. Baada ya muda watu waliokubali kuingia kwenye uwekezaji ule walipata faida kubwa sana. Alisema anajutia sana fursa hiyo aliyoipoteza na anaona ni bahati ambayo ilimponyoka.

Baada ya maelezo haya Arkad alitoa ufafanuzi kwamba kama mtu huyu angechukua hatua na kufanya uwekezaji ule angepata faida kubwa sana.

Arkad aliuliza kama kuna mtu mwingine ambaye ana uzoefu wa bahati kumponyoka. Alisimama mtu mwingine na kusema yeye ni mnunuzi wa wanyama, ananunua mbuzi, ngamia na kadhalika. Aliendelea kusema kwamba wakati fulani alisafiri kwenda maeneo ya mbali ili kutafuta wanyama, hawakupata wanyama wengi sana ila waliporudi ilikuwa ni usiku na hivyo milango ya babeli ilikuwa imefungwa. Hii iliwalazimu kukesha nje wakisubiri milango ifunguliwe ndio waweze kwenda kuuza wanyama wao. Usiku huo mfanyabiashara mwingine wa wanayama alimfuata na kumwambia amepata dharura mke wake ni mginjwa hivyo ianabidi aondoke haraka. Akaomba amuuzie wanyama wake kwa bei ndogo ili aweze kupata fedha na kuondoka. Alikubali ila akasisitiza mpaka ahesabu wanyama wale ndio angetoa fedha. Haikuwezekana kuhesabu wanyama wale usiku ule, hivyo mtu yule akamuomba amlipe sehemu ya malipo na inayobaklia atamalizia akishahesabu asubuhi, ila bado alisita kufanya maamuzi. Ilipofika asubuhi na milango kufunguliwa walijitokeza wanunuaji wa wanyama na kununua wanyama wale kwa bei mara tatu ya aliyokuwa anataka kuuziwa. Alisema hiyo ni bahati ambayo iliacha na ikapotea.

Arkad alisema hii ni hadithi ya kipekee sana. Aliuliza ni kitu gani ambacho watu wamejifunza kwenye hadithi zile. Mtu mmoja alisema kwamba watu wale walikosa fursa kwa sababu ya tabia ya kuahirisha mambo au kusita kufanya maamuzi.

Arkad alisema ni kweli kabisa na akasema kwa miaka mingi amekuwa akishuhudia watu wakipitwa na fursa kwa sababu ya kusita kufanya maamuzi. Aliwaambia fursa zinakuja sawa kwa watu wote ila wale wanaochukua hatua mapema ndio wananufaika na fursa hizo. Wale wanaosita sita wanaachwa nyuma na kuendelea kuwa masikini.

Arkad alisema kutokana na mjadala huu tunakubaliana kwamba bahati sio kitu ambacho kinakuja tu au kinaombwa bali ni pale mtu anapoiona fursa na kuchukua hatua mara moja. Aliwaambia matendo ndio yatawaletea mafanikio wale wanaoyatamani.

Tushirikishe kwenye maoni hapo chini wewe binafsi una maoni gani kuhusu bahati? Je umewahi kupata bahati ambayo imekuja tu? Au unafikiri ukifanya nini ndio unaweza kutengeneza bahati? Karibu kwa maoni ili tujifunze zaidi.

Nakutakia kila la kheri katika kufikia uhuru wa kifedha.

TUPO PAMOJA.