Rodan aliyekuwa mtengeneza spea wa babeli alikuwa na vipande hamsini vya dhahabu. Alitembea njiani kwa maringo huku dhahabu ikitikisika kwenye mifuko yake. Haijawahi kutokea kwenye maisha yake akawa na kiasi kikubwa vile cha dhahabu. Kiasi hiko cha dhahabu kingemwezesha kununua chochote alichokuwa anataka iwe ni ardhi, nyumba, farasi na kadhalika.
Jioni hiyo Rodan aliingia kwenye duka la Mathon ambaye alikuwa mkpopeshaji wa dhahabu na pia kuuza madini ya thamani. Rodan alifika mbele ya Mathon na kumwambia anahitaji ampe ushauri wa kitu gani anaweza kufanya. Mathon alimshangaa na kumuuliza ni maswahiba gani yamempata mpaka akaombe ushauri kwa mkopesha dhahabu(fedha), alimuuliza kama amepoteza fedha kwenye kamari na hivyo amekuja kukopa ili akacheze tena. Rodan alimjibu hapana, hajafata kukopa fedha bali anatafuta ushauri wa busara.
Mathon alimwambia Rodan kwamba haamini anachokisikia kwamba mtu anakwenda kuomba ushauri kwa mkopeshaji wa fedha. Alimwambia watu huja kwake kukopa fedha tu na kulipa, ila ushauri wake ahwataki. Na akamuambia hakuna mtu anayeweza kutoa ushauri mzuri kama mkopesha fedha.
Mathon alimkaribisha Rodan na akamwambia kwamba watakula chakula pamoja jioni hiyo iliw aweze kuongea vizuri. Baada ya kukaa Mathon aliuliza, sasa niambie ni tatizo gani unalo? Rodan alimjibu kwamba ni zawadi ya mfalme. Alimwambia kwamba alimtengenezea mfalme kitu kizuri ambacho alikipenda sana na hivyo akamzawaidia vipande hamsini vya dhahabu. Alimwambia kwamba kwa sasa hajui afanye nini na kiasi hiko kikubwa cha dhahabu. Alimwambia watu wengi wamekuwa wakimpa mawazo ya kutumia fedha hiyo na wengine wanataka awasaidie. Mathon alimwambia hiko ni kitu cha kawaida kwamba mtu anapokuwa na hela watu wake wakaribu wanategemea kunufaika na fedha hizo, kwa sababu watu wanapenda fedha zinazopatikana kirahisi.
Rodan aliendelea kusema kwamba mume wa dada yake anayeitwa Araman ndio anamsumbua zaidi. Alisema Araman anatamani kuwa tajiri hivyo anamwomba amkopeshe dhahabu ili akafanyie biashara. Mathon alimwambia umeleta mjadala mzuri,mtu anapopata fedha majukumu yake yanaongezeka na wanaomzunguka wanamwangalia kwa jicho la tofauti. Alimwambia pia fedha huleta hofu kama ikipotea na mtu akarudi kwenye umasikini na pia huleta nguvu ya kuweza kufanya mambo mengi. Lakini pia fedha huleta fursa za kuweza kufanikiwa zaidi.
Mathon alimweleza hadithi moja ya mkulima wa Ninev aliyekuwa na uwezo wakusikia lugha za wanyama. Alisema mkulima huyu siku moja jioni alikuwa pembeni ya shamba na akasikia wanyama wakizungumza. Ng’ombe wa kulima alikuwa anamwambia farasi kwamba yeye ng’ombe anafanya kazi siku nzima iwe kuna jua au la ila wewe farasi unapumzika na kumbeba tu bwana wetu. Alimwambia wewe farasi unakula raha, ikiwa bwana haendi mahali basi wewe unakula tu majani na kupumzika. Farasi alimwangalia maksai yule kwa huruma na kumwambia kama unaona hivyo kesho nitakusaidia njia unayoweza kutumia kupata mapumziko. Wakati watumwa wanakuja kukuchukua ili ukalime, lala chini uonekane unaumwa. Ukifanya hivyo watakuacha na hivyo utapumzika.
Maksai yule alifuata ushauri ule na kesho yake watumwa walienda kwa Mwenye shamba na kumwambia maksai anaumwa na hivyo hawezi kufanya kazi. Yule bwana aliwaambia fungeji jembe kwenye farasi akalime maana kazi haiwezi kulala. Farasi alifungwa jembe na kufanya kazi siku nzima. Farasi yule alifikiri anamsaidia rafiki yake kumbe amejiingiza kwenye matatizo makubwa yeye mwenyewe. Farasi aliporudi kwenye banda jioni akiwa amechoka sana maksai alimpokea na kumwambia wewe ni rafiki mwema leo nimepumzika vizuri sana. Farasi alimwangalia kwa hasira na kumwambia ametoa ushauri ambao umemuumiza yeye mwenyewe. Alimwambia maksai aamke kesho yake akafanye kazi yake maana amesikia wakisema kwamba kama ataendelea kuumwa watamchinja. Baada ya pale hawakuongea tena na urafikiw ao ukawa umeishia pale.
Baada ya kumaliza hadithi hii Mathon alimuuliza Rodan, umejifunza nini kutoka kwenye hadithi hii?
Na mimi nakuuliza umejifunza nini kutoka kwenye hadithi hii? Tushirikishe kwenye maoni hapo chini.
Tutaendelea na sehemu hii ya uchambuzi kwenye makala ijayo.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa.
TUPO PAMOJA.
Usisahau kutushirikisha ulichojifunza kwenye hadithi ya maksai na farasi.
Nilichojifunza kwenye hadithi ni kwamba 1:Tunapomtafuta mshauri wa jambo lolote lile tumtafute anayejua na mwenye uzoefu katika jambo hilo.2.Kama we ni mshauri wa watu toa ushauri unaojenga badala ya kubomoa mfano.farasi alimshauri ng’ombe ajifanye anaumwa ili asifanye kazi, kitu ambacho ni hatari kwenye uzalishaji wa mkulima na hatari hiyo ilimgeukia yeye. 3.Tupende kazi zetu. Tukifanya kazi tunazo zipenda hatutakua tunafanya kazi bali tunacheza mchezo tunaofurahia.Hatutaona kamwe ugumu wa kazi. Vilevile nimejifunza kuwa fedha huleta hofu kama ikipotea na mtu akarudi kwenye umasikini(tunahitaji kuwa na nguvu ya kutawala fedha badala ya kuhofia,nilielewa vizuri kwenye kitabu Rich Dad Poor Dad.
LikeLike
Asante sana Ngutiti.
LikeLike
Katika hadithi hii, nimejifunza kwamba, unaweza kufanya jambo la hatari ukidhani litawaumiza wengine kumbe linaweza kukuumiza pia, ni muhimu kuepuka kupokea ushauri usiyofaa kwenye maisha yetu, Kama tukipata nafasi ya kuwashauri wengine basi tuwape ushauri unaofaa, kuchagua kuwa wazembe kwenye kazi zetu hakumuumizi mwajiri pekee Bali hata sisi wenyewe. Uvivu haujawahi kumwacha salama mtu; kuna wakati utafika atapokea malipo ya uvivu wake.
LikeLike