Tunaendelea na uchambuzi wa kitabu THE RICHEST MAN IN BABYLON.
Mji wa babeli ulikuwa umezungukwa na ukuta imara sana na ambao ulikuwa na mlango imara wa chuma. Ukuta huu uliweza kuulinda mji wa babeli dhidi ya wavamizi ambao wangeweza kuja kuchukua utajiri wa babeli.
Kuna kipindi babeli ilivamiwa na majeshi kutoka maeneo mbalimbali. Majeshi haya yalizunguka ukuta wa babeli na walikuwa kwenye mlango mkuu wakipambana kuingia. Kipindi hiki jeshi kuu la babeli lilikuwa limesafiri na mfalme. Ndani ya ukuta wa babeli wananchi wengi walikuwa na wasi wasi mkubwa ni nini kitatokea ikiwa majeshi yale yangefanikiwa kuingia.
Juu ya ukuta zilisikika sauti za majeshi yakizunguka na kubomoa ili kupata nafasi ya kuingia ndani ya babeli. Wanajeshi wa babeli nao walikuwa wakipambana nao japo wengine walikufa katika mapambano hayo. Uvamizi huo ulikuwa mkali sana na kitu pekee ambacho kingeweza kuwaokoa babeli na kuta zile zisiweze kuvunjwa na wavamizi wale.
Banzar ambaye alikuwa ni mwnajeshi, ndio alikuwa chanzo kikuu cha habari za uvamizi huo kwa wananchi wengine. Yeye ndio alikuwa akipata habari ya nini kinaendelea na watu wengi walimfuata kumuuliza hatima ya uvamizi ule. Mzee mmoja mfanyabiashara alimfuata na kumwambia, hebu niambie wavamizi hawa hawataweza kuingia? Maana mwanangu amesafiri na mfalme na mke wangu ni mzee na anaumwa hivyo siwezi kumlinda. Na pia kama wavamizi hawa watafanikiwa kuingia wataiba vitu vyangu vyote kwenye biashara na hivyo kupata hasara kubwa. Alimwambia sisi ni wazee hatuwezi kupigana na pia hatuwezi kuchukuliwa kama watumwa, tutakufa tu. Niambie kama watu hawa wahataweza kuingia. Banzar alimwangalia na kumwambia usiwe na hofu, ukuta wa babeli ni imara. Nenda nyumbani na mwambie mke wako ukuta wa babeli utawalinda nyie na mali zenu kama unavyolinda utajiri wa mfalme.
Baada ya mzee yule kuondoka alikuja mama mwingine akiwa amebeba mtoto alimfuata Banzar na kumwambia, tafadhali tupe habari za ukweli, tuambie ni nini kitatokea ili niweze kumwambia mume wangu ambaye anaumwa na hajiwezi. Banzar alimwambia usiwe na hofu, ukuta wa babeli ni imara na utawalinda wote dhidi ya wavamizi hawa. Alimwambia nenda kamwambie mume wako kwamba ukuta wa babeli ni imara na hauwezi kuvunjwa na wavamizi.
Watu wengi waliaendelea kumfuata Banzar na kumuuliza kuhusiana na uvamizi na wote aliwajibu kwamba ukuta wa babeli ni imara na hivyo utawalinda wananchi wote na mali zao dhidi ya wavamizi.
Kwa wiki tatu na siku tano uvamizi ule ulikuwa ukiendelea, wanajeshi walizunguka ukuta na kila siku kulikuwa na kelele za mapambano. Baada ya siku ya tano ya wiki ya tatu sauti zile zilipotea na hivyo uvamizi ule kuwa umeshindikana. Wananchi walitoka kwenye nyumba zao na kushangilia sana kwamba hawajaweza kuvamiwa na majeshi yale.
Ukuta wa babeli uliweza kuwalinda wananchi wake na mali zao dhidi ya uvamizi. Babeli iliweza kudumu imara kwa muda mrefu kwa sababu ilikuwa na ulinzi imara na sio vinginevyo.
Tunajifunza nini hapa?
Ukuta wa babeli ni mfano imara wa uhitaji mkubwa wa ulinzi wa mali na fedha zetu. Unahitaji kuwa na ulinzi imara sana wa mali na fedha zako la sivyo zitachukuliwa na wavamizi. Na dunia ya sasa ina wavamizi wengi sana na wengine huwezi kuwajua kabisa.
Baadhi ya kuta imara unazoweza kujenga ili kulinda mali zako na fedha ni;
1. Kuwa na bima ya vitu mbalimbali.
2. Kuwa na akiba ambayo ipo sehemu salama.
3. Kuwekeza katika uwekezaji imara na unaoaminika.
Fanyia kazi jambo hili la kuweka ulinzi katika mali na fedha zako ili kuepuka kurudishwa nyuma na wavamizi.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia uhuru wa kifedha.
TUPO PAMOJA.
Thanks Alot Amani,Be blessed Alot a man of Vision!
LikeLike
Thank you.
LikeLike
AHSANTE MUNGU AKUBARIKI
LikeLike
Asante na karibu sana.
LikeLike
nzuri sana hii
LikeLike
Vizuri
LikeLike