KITABU; The 4 Hour Work Week, Jinsi Ya Kujitengenezea Uhuru Wa Kweli.

Katika ulimwengu wa sasa, vitu viwili ambavyo vinaashiria uhuru wa kweli ni muda na fedha. Unakuwa huru pale ambapo unaweza kupanga ufanye nini na muda wako. Na pia unakuwa huru pale ambapo unaweza kupata kipato kinachotokana na juhudi na maarifa yako.

4 HOUR

Lakini cha kushangaza asilimia kubwa ya watu hawana kabisa uhuru. Haijalishi wanafanya kazi gani na wanamfanyia nani kazi, watu wengi wanakosa uhuru wa muda na pia wanakosa uhuru wa fedha.

Kwa upande wa walioajiriwa hili halina ubishi wowote, muda wa mwajiriwa uko chini ya aliyemuajiri. Mwajiriwa atakuwa kazini kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni bila ya kujali ana kazi ya maana anayofanya au la. Kwa mpango huu wafanyakazi wengi wanakujikuta wanapoteza muda mwingi kwenye siku zao huku wakizalisha kidogo sana. Na uhuru wa fedha kwenye kuajiriwa haupo. Hii ni kwa sababu sio wewe mwenyewe unayoamua ulipwe kiasi gani na hata kama mwanzoni uliweza kushawishi hivyo, baadae utaendelea kupewa kiasi ambacho hakilingani na uzalishaji wako.

Kutokana na kukosekana kwa uhuru halisi kwa walioajiriwa unaweza kufikiri waliojiajiri au wanaofanya biashara ndio wana uhuru huo halisi! Sio kweli, hawa ndio wanaweza kuwa wamekosa uhuru zaidi. Hii ni kwa sababu watu wengi waliojiajiri wanakuwa wanafanya kazi karibu muda wote, hata kama hayupo kwenye kazi yake hiyo bado atakuwa anaendelea kuwa na mawazo na mawasiliano kuhusiana na kazi yake. Kwa hali hii muda wake unakuwa unamilikiwa na bishara yake au wateja wake. Uhuru wa fedha anaweza kuwa nao lakini nao sio uhuru halisi, ukilinganisha na jinsi biashara yake inavyommiliki.

Hivyo kwenye ukosefu wa uhuru wa muda na fedha, aliyejiajiri hawezi kumcheka aliyeajiriwa. Wote hawana tofauti kubwa.

Ni kutokana na ukosefu huu mkubwa wa uhuru ndio mwandishi Tim Ferris akaandika kitabu The 4 Hour Work Week. Lengo kubwa la kitabu hiki ni kumpatia mtu uhuru wa muda na uhuru wa fedha pia.

Mwandishi anasema kwamba unaweza kutoka kwenye kufanya kazi masaa 40 kwa wiki(masaa nane kila siku kwa siku tano) mpaka kufanya kazi masaa 4(manne) kwa wiki(saa moja kila siku kwa siku nne), na ukawa na uzalishaji mkubwa kuliko ulionao sasa.

Mwandishi ametoambinu nyingi sana za kuongeza ufanisi wako kama umeajiriwa au umejiajiri. Ameelezea mambo ambayo ni muhimu wewe kufanya na mambo gani uyafute kabisa kwenye muda wako wa kazi ili uweze kumaliza majukumu yako kwa muda mfupi zaidi.

Na pia mwandishi ameelezea jinsi gani mtu unaweza kuwa na uhuru wa kweli kwa muda wake na fedha zake. Anasema kufanya kazi miaka 40 ndio uje ustaafu ni kukosa kabisa uhuru. Badala yake anaonesha ni jinsi gani ya kupata kustaafu kila baada ya muda mfupi na baadae kuendelea na majukumu yako(mini retirement).

Mwisho kabisa mwandishi amejadili baadhi ya biashara ambazo unaweza kuzianzisha hata kama umeajiriwa na zikakupa uhuru mkubwa sana wa muda na fedha. Amechambua biashara hizo vizuri sana kiasi kwamba ni wewe tu kufanya maamuzi ya kuanza kuzifanya na kuanza safari yako ya kudai uhuru wako.

Pata kitabu hiki na ukisome na kisha yafanyie kazi yale utakayojifunza na hakika utaanza kutengeneza uhuru wako.

Kupata kitabu hiki bonyeza maandishi haya na uweke email yako kisha utatumiwa email yenye link ya kitabu. Email hiyo pia itakuwa na link za vitabu vingine vizuri.

Usikose nafasi hii adimu ya kujiletea ukombozi wa maisha yako.

Mwandishi anasema; unao uhuru ambao umeupigania. Hivyo kama hutafanya chochote kudai uhuru wako, hakuta atakayekupatia na maisha yataendelea kuwa magumu kila siku.

Nakutakia kila la kheri kwenye kujitengenezea uhuru wa kweli.

TUPO PAMOJA.

Makirita Amani – makirita@kisimachamaarifa.co.tz 0717396253

kitabu-kava-tangazo4323

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: