Ni utaratibu wetu hapa kwenye KISIMA CHA MAARIFA kila alhamisi na ijumaa kuwa na uchambuzi wa vitabu. Na wiki iliyopita tulimaliza uchambuzi wa kitabu THE RICHEST MAN IN BABYLON
Kuna mambo mengi sana tumejifunz akupitia kitabu hiki ambapo kama utaanza kuyafanyia kazi mapema basi maisha yako ni lazima yatabadilika.
Pia kabla ya kitabu hiki tulifanya uchambuzi wa kitabu RICH DAD POOR DAD ambapo pia tulijifunza mbinu nzuri sana za kuweza kufikia mafanikio kupitia kile tunachofanya.
Wiki hii hatutaanza kitabu kingine mpaka wiki ya pili ya mwezi wa kwanza. Hii ni kutokana na likizo fupi tutakayokuwa nayo kwa ajili ya kujiandaa zaidi na mwaka 2015 ili kuweza kukuelimisha na kukuhamasisha zaidi.
Unaweza kutumia muda huu kupitia makala zote za uchambuzi zilizopita na kupanga ni mambo gani uliyojifunza kwneye vitabu hivi unayoweza kuyafanya mwaka 2015 ili kuboresha zaidi kazi zako na biashara zako.
Naamini tutaendelea kuwa pamoja ili kuboresha maisha yetu zaidi.
Nakutakia kila la kheri.