Mwaka 2014 ndio umeisha na sasa tunakaribia kabisa kuuanza mwaka 2015. AMKA CONSULTANTS tunatumia nafasi hii kukushukuru sana wewe kwa kuwa pamoja na sisi mwaka huu 2014 kwa kujifunza, kuhamasika na hata kupata ushauri ambao kwa namna moja au nyingine uliweza kukusaidia.

Pia tunashukuru kwa shuhuda na maoni mazuri yanayoendelea kutolewa na wasomaji mbalimbali. Tunapata muitikio mzuri sana kutoka kwa wasomaji ambao wametushirikisha ni jinsi gani AMKA MTANZANIA imeweza kubadili maisha yao na pia ni mamo gani wangependa yaongezwe. Tunawaahidi kwamba tutafanyia kazi yale yote yaliyopo ndani ya uwezo wetu.

Kama bado hujapata nafasi ya kutoa ushuhuda na maoni yako tafadhali bonyeza maandishi haya na ujaze fomu, ni zoezi linalochukua muda mfupi sana. Tunashukuru sana kwa ushirikiano mkubwa unaoendelea kutuonesha.

Makala zilizosomwa sana mwaka huu 2014.

Mwaka huu 2014 umekuwa mwaka ambao wasomaji wa AMKA MTANZANIA wameongezeka mara dufu. Hapa ni makala ambazo zimesomwa sana mwaka huu 2014. Unaweza kuzisoma tena ili kuendelea kujifunza na kuhamasika.

1. Huyu Ni Kijana Wa Kitanzania Aliyeanza Biashara Kwa Mtaji wa Milioni Nne na Baada Ya Miaka Mitatu Ana Zaidi Ya Milioni Mia Moja.

2. Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutengeneza Pesa Zako Na Kuwa Tajiri.

3.  Kama Una Tabia Hizi 30 Tayari Wewe Ni Mjasiriamali, Chukua Hatua.

4. Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu Moja.

5.  Leo Nakuwa Mganga Wako; Kama Una Tabia Hizi Tano Huwezi Kufanikiwa Kamwe.

6. Njia Sita(6) Za Kudhibiti Matumizi Yako Katika Biashara .

7. Kitabu; Richard Branson–Mafunzo Ya Maisha(Screw It, Lets Do It).

8. Kama Una Tabia Hii Moja Una Uhakika wa Zaidi ya 90% Wa Kufanikiwa Kwenye Chochote Unachofanya.

Zawadi Ya Kitabu.

Katika mwaka huu 2014 AMKA CONSLULTANTS tumekushirikisha vitabu vingi sana na vizuri. Pia tumeanzisha kundi la kusoma vitabu kwa pamoja linalojulikana kama Tanzania Voracious Readers ambapo kupitia kundi hili tunasoma vitabu viwili kila wiki na lengo ni kusoma vitabu 500 ndani ya miaka mitano. Kama unataka kuingia kwenye kundi hili, weka application inayoitwa Telegram Messenger kwenye simu yako kisha nitumie ujumbe kwa application hiyo kwenye namba 0717396253. Ili kuingia na kubaki kwenye kundi hili unahitaji kweli ufanye kazi hiyo ya kusoma, vinginevyo utaondoka.

Hapa tunakupatia zawadi ya kitabu kizuri sana unachoweza kukisoma kwa kumalizia mwaka.

Kitabu hiki tunachokuzawadia hapa kinazungumzia mabadiliko na jinsi ya kwenda nayo ili usiachwe nyuma. Tunaishi kwneye dunia inayobadilika kwa kasi sana na hivyo ukichelewa unaachwa nyumba.

Kitabu hiki kinaitwa WHO MOVED MY CHEESE, ni kitabu kifupi sana na kina kurasa 32 tu. Lakini kurasa hizi zimejaa busara kubwa unayoweza kuanza kuitumia sasa na ukabadili maisha yako kwa kiwango kikubwa sana. Unaweza kumaliza kukisoma ndani ya saa moja.

Kupata kitabu hiko bonyeza maandishi haya.

Washirikishe marafiki zako watano.

Nina ombi moja muhimu sana kwako. Kwa kuwa wewe umekuwa unanufaika na makala unazosoma hapa kwenye AMKA MTANZANIA kila siku, naomba uchukue nafasi ya leo kuwashirikisha marafiki au jamaa zako ambao unajua hawaijui AMKA MTANZANIA. Najua umekuwa unafanya hivyo kila siku, lakini leo nakuomba uwashirikishe makala hii kwa sababu ina makala zote ambazo zilisomwa sana mwaka jana na zinaweza kumsaidia mtu anayezisoma wakati wowote.

Hivyo makala hii itume kwa watu watano ambao unafikiri hawajawahi kukutana na AMKA MTANZANIA, itume kwenye email zao au watumie link ya makala hii kupitia mitandao kama facebook, wasap na mingine mingi. Wasisitize wapitia mtandao huu kwa sababu kuna mengi ya kujifunza. Asante sana kwa kufanya hivi, kwa sababu unakuwa balozi wa kuwasaidia wengi zaidi.

Likizo fupi.

Kama tulivyotoa taarifa kwenye makala ya jumatatu, wiki ijayo AMKA CONSULTANTS tutakuw alikizo kwa wiki moja. Likizo itaanza tarehe 22/12/2014 mpaka tarehe 28/12/2014. Katika kipindi hiki hakutakuwa na makala mpya katika mitandao yote inayoendeshwa na AMKA CONSULTANTS. Ila utapata nafasi ya kuendelea kusoma makala hizi za nyuma na hata vitabu ulivyotumiwa.

Likizo hii itatuwezesha kujiandaa kukuhudumia vizuri mwaka 2015.

Tunashukuru sana kwa ushirikiano unaoendelea kutuonesha na tunaomba uendelee zaidi mwaka 2015 pamoja na kuwaalika wote unaowajua watembelee AMKA MTANZANIA na pia kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Usisahau kubonyeza hapa na kujaza fomu ili kutupatia ushuhuda na maoni yako.

TUPO PAMOJA.

kitabu-kava-tangazo4322