Safari ya kufikia mafanikio sio rahisi kama ambavyo wengi wanafikiri. Ni safari ambayo inaweza kuwa ngumu sana hasa pale unapozungukwa na jamii ambayo haioni kile unachokiona wewe. Ili kufikia mafanikio ni muhimu sana wewe kuweka malengo na mipango yako na kisha kuifanyia kazi bila ya kukata tamaa hata kama mambo yanakuwa magumu kiasi gani.

Pamoja na malengo na mipango yako hiyo kuna mambo mengine ambayo unapaswa kuyasisitiza na kuyang’ang’ania ili safari yako ufike salama. Hapa tutajadili mambo 15 muhimu ya kunga’ng’ania ili kuwez akufikia mafanikio;

1. Ng’ang’ania kutimiza malengo yako.

Kwa watu wengine malengo yako yanaweza kuonekana kama mchezo au ndoto za mchana au kitu kisichowezekana kabisa. Usiwasikilize, mara nyingi hawajui walisemalo mpaka waone limetokea. Ng’ang’ania kutimiza ndoto zako ili kuboresha maisha yako.

2. Ng’ang’ania kuwa mkubwa zaidi.

Kwa kile unachofanya hakikisha unakifanya kwa kuleta picha kwamba wewe unajua unachofanya. Fanya kwa ubora zaidi na ongea kwa kujiamini. Kwa kunga’ng’ania kuwa mkubwa zaidi utajiongeze akujiamini na hii itakuwezesha kufikia mafanikio makubwa.

3. Ng’ang’ania kusamehe.

Kama kuna mtu yeyote ambaye alikukosea msamehe na endelea na maisha yako. Usipoteze maisha yako kwa kuweka kinyongo na mtu hata kama amekufanyia nini. Ng’ang’ania kusamehe kila mtu ili wewe ubaki na moyo mweupe wa kuweka juhudi zaidi kwenye shughuli zako na kuweza kufikia mafanikio makubwa.

4. Ng’ang’ania kuiona glass imejaa maji nusu.

Kama ukiwekewa glass ambayo ina maji na kuulizwa unaona nini hapo kuna majibu mawili, unaweza kuona glass ambayo iko tupu nusu au unawez akuona glass ambayo ina maji nusu. Wewe ng’ang’ania kuona glass imejaa nusu. Kwa maana rahisi mara zote una upande chanya wa jambo lolote. Kila jambo ng’ang’ania kuona upande ambao ni chanya ambapo utajifunza zaidi kuliko ukiangalia upande ambao ni hasi.

5. Ng’ang’ania kuwa mkweli kwako mwenyewe.

Mawazo yako ndio yanayojenga tabia zako. Hivyo unapokuwa na mawazo mazuri moja kwa moja utajenga tabia nzuri ambazo zitakuletea mafanikio. Watu wanaweza kukuona vyovyote wanavyotaka, ila wewe kuwa mkweli kwako wewe binafsi. Amua kuwaza mawazo ambayo yatakufanya uweze kufikia mafanikio, usijidanganye hata kidogo.

6. Ng’ang’ania kuzungukwa na watu ambao wanakufanya ukue zaidi.

Wewe ni wastani wa watu watano wanaokuzunguka. Ukizungukwa na wazembe watano, wewe utakuwa mzembe wa sita. Ukizungukwa na watu wenye mafanikio watano, wewe utakuwa mwenye mafanikio wa sita. Wanaokuzunguka wana nguvu kubwa sana kwako hivyo hakikisha wanakwenda kule unakotaka kwenda wewe ili muweze kufika pamoja.

Kusoma mambo mengine tisa muhimu yaliyobakia jiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza maandishi ya neno KISIMA CHA MAARIFA, jaza fomu na kisha tuma ada ya uanachama kwenye namba 0717396253/0755953887 kumbuka kutuma pia email ambayo umejiunga nayo ili uanachama wako uweze kudhibitishwa.

Nakutakia kila la kheri kwa mwaka huu 2015.

TUPO PAMOJA.

kitabu-kava-tangazo4322