Kwa wewe kuwa tayari kusoma na kujifunza kupitia kitabu hiki ina maana kwamba unahitaji elimu hii muhimu itakayoboresha maisha yako. Na ili uweze kupata elimu hii na iweze kukusaidia ni lazima uwe tayari kuvpokea vile unavyojifunz ana kuvifanyia kazi. Pia ni lazima ufuate maelekezo yote unayojifunza. Ukichagua kufuata baadhi na kupuuza baadhi haitakusaidia na utakuwa umepoteza vyote ulivyojifunza.

Muhtasari wa jinsi ya kutengeneza masharti utakayokuwa unapeleka kwenye akili yako ya ndani ili iweze kukuletea mazingira ya kufikia utajiri.

HATUA YA KWANZA;

Nenda kwenye sehemu ambayo imetulia(sehemu nzuri inaweza kuw akitandani usiku) ambapo hutasumbuliwa na kitu chochote. Funga macho yako  na sema yale maneno ambayo uliyaandika kwenye hatua zile sita tulizojifunza. Sema kiasi cha fedha unachotaka, tarehe ya mwisho ya wewe kupata kiasi hiko na bidhaa au huduma unayotegemea kutoa ili kupata fedha hizo. Wakati unafanya hivi jione tayari unamiliki fedha hizo unazotaka.

Kwa mfano kama unataka kupata milioni hamsini kwa mwaka mmoja ujao, na utakuwa unatoa huduma ya uuzaji(salesman), tamko lako litakuwa hivi;

Mpaka kufikia january 30 mwaka 2016 nitakuwa nimepata milioni 50 ambazo zitatoka kwenye vyanzo mbalimbali katika kipindi hiki.

Katika kupata fedha hii, nitatoa huduma ya hali ya juu sana ambayo iko ndani ya uwezo wangu katika eneo la uuzaji. Na nitauza huduma ambazo ni bora sana kwa yule atakayezitumia.

Naamini kwamba nitakuwa nazimiliki hizi fedha. Imani yangu ni kali sana kiasi kwamba sasa hivi naziona fedha hizi mbele ya macho yangu. Naweza kuzishika kw amikono yangu, zinasubiria kuhama na kuja kwangu muda utakapofika. Tayari ninao mpango wa kuzipata fedha hizi na sasa naufuata mpango huo.

HATUA YA PILI;

Rudia maelezo hayo asubuhi na jioni mpaka yatakapokuwa sehemu ya mawazo yako yako na uweze kuona kama ndio kitu kinachotokea kwenye maisha yako.

HATUA YA TATU;

Weka nakala ya maelezo yako haya sehemu ambayo unaweza kuyaona asubuhi na usiku na isome kabla ya kulala na pale unapoamka mpaka.

Kumbuka unapofuata maelekezo haya unaijenga akili yako ya ndani kuweza kukuletea wewe kile ambacho unakifikiria kwa muda mrefu.

Mwanzoni maelekezo haya unaweza kuona ni ya ajabu, lakini usikubali hili likuzuie. Fuata maelekezo hata kama utayaona ya ajabu kiasi gani, jinsi utakavyozidi kuyafuata, yatazidi kujenga nguvu na ulimwengu mpya utafunguka kwako.

Wasi wasi ni tabia ya tabia ya kila binadamu hasa linapokuja jambo ambalo ni jipya. Lakini kama utafuata maelekezo haya na kufanya kwa imani utafikia hatua ambayo wewe utakuwa ndio kiongozi wa maisha yako.

Maelekezo yote yaliyotolewa hapa yanatakiwa kufuatwa kwa ung’ang’anizi. Yasiachwe kwa sababu matokeo ya haraka hayajaonekana.

Nakutakia kila la kheri katika maisha mapya ya mafanikio makubwa ambayo umeanza kuyaishi.

TUPO PAMOJA.