Moja ya kauli za kusikitisha sana ninayokutana nayo kwa watu ni kwmaba, najaribu kufanya hii biashara nione kama itanipa faida.
Kwa kauli hii tu tayari umeshashindwa kwenye biashara unayotaka kufanya.
Biashara haijaribiwi, ila inafanywa. Unaposema unajaribu biashara maana yake unaifanya kwa majaribio tu na kama majaribio yako yatakwenda vizuri utaendelea ila kama majaribio yako yatakwenda vibaya utaachana nayo.
SOMA; Unapokuwa Tayari Kuingia Kwenye Ujasiriamali Fanya Vitu Hivi Vitano.
Sasa nina kitu kimoja ninachoweza kukuhakikishia, majaribio yako yatakwenda vibaya na kwa kuw aupo kwenye majaribio utaondoka kwenye biashara hiyo. Kila kitu kwenye maisha kina changamoto na matatizo yake. Biashara ndio kabisa ina changamoto nyingi sana hasa kwa wale wanaoanza kabisa.
Kama unaingia wkenye biashara kwa kujaribu, utakapokutana na changamoto hizi, utakimbia. Na mbaya zaidi utakapokwenda kujaribu tena biashara nyingine, utakutana na changamoto na utaacha pia.
Badala ya kujaribu biashara hebu fanya biashara. Jitoe kwamba hii ndio biashara utakayofanya kwenye maisha yako. Weka nguvu zako zote, weka akili zako zote na weka kila ulichonacho kwenye biashara hii. Kwa hali hii hata ukikutana na changamoto utazivuka na utafikia mafanikio makubwa.
Usijaribu biashara, fanya biashara.
SOMA; Weka Pamoja Vitu Hivi Vitatu Na Tayari Wewe Ni Mjasiriamali Mwenye Mafanikio Makubwa.