USHAURI; Hii Ndio Changamoto Kubwa Inayokuzuia Wewe Kutatua Changamoto Zako.

Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA. Karibu tena kwenye kipengele hiki cha ushauri wa changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yetu. Kila siku ya jumatatu tunaangalia changamoto moja ambayo inakuwa imeletwa kwetu na ninyi wasomaji na tunashauriana ni jinsi gani ya kuweza kupambana na changamoto hii na kusonga mbele.

Kwa siku ya leo hatutakuwa na changamoto moja kutoka kwa msomaji bali tutaangalia changamoto moja inayowakabili watu wengi ambao wapo tayari kubadili maisha yao.

Kupitia kazi hii ya uandishi na uhamasishaji nimepata bahati ya kukutana na watu wengi sana. Nimekuwa nikikutana ana kwa ana na wasomaji ambao wamekuwa wakihitaji ushauri katika mambo mbalimbali wanayopitia kwneye maisha yao, au wanayotaka kufanya kwenye maisha yao.

SOMA; Biashara Unayofanya Sasa, Au Utakayoanza Sasa Sio Biashara Utakayofanya Milele.

Tumekuwa tukipata nafasi nzuri ya kuzungumza na kuchambua mambo mbalimbali yanayohusiana na changamoto ambazo watu hawa wanapitia.

Katika kukutana huku na kuzungumza na watu mbalimbali nimejifunza kitu kimoja muhimu sana ambacho kinakuwa kikwazo juu ya vikwazo ambavyo tayari watu wanavyo. Yaani tayari mtu ana matatizo au changamoto na anataka kuitatua ila kunakuwa na changamoto nyingine kubwa ambayo inamzuia kutatua changamoto hiyo wanayotaka kuitatua. Na kwa bahati mbaya sana changamoto hii nyingine kubwa watu wengi wanakuwa hawaioni. Hii inaifanya changamoto hii kuwazuia wengi kuweza kufikia mabadiliko waliyokuwa wanatarajia kwenye maisha yao.

Kwenye makala ya leo utapata nafasi ya kujua changamoto hii na jinsi ya kukabiliana nayo. Nina hakika ukiweza kushinda changamoto hii moja hakuna kinachoweza kukuzuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Utaweza kubadili maisha yako hata kama ni mabaya kiasi gani na utaishi maisha unayoyafurahia.

SOMA; Jambo Muhimu La Kufanya Wakati Unapia Magumu.

Je ni changamoto gani hii ambayo inawazuia wengi kuweza kubadili maisha yao?

Changamoto hii tunayoijadili leo na inayowazuia wengi kuweza kubadili maisha yao ni kutaka mabadiliko hayo yatokee haraka sana. Yaani mtu anataka kwa kuwa sasa ameshaamua maisha yake yawe tofauti na yawe bora basi aanze kuona majibu haraka.

Hiki ni kitu ambacho nimekuwa nakipata kwa watu wengi ambao ninakutana nao kwa ajili ya ushauri. Watu wengi wanakuwa na shauku kubwa na wanapenda kuuliza ni njia gani wakitumia matatizo yao yataisha haraka na maisha yao yataanza kuwa bora. Wamekuwa wakiwa na mawazo kwamba kuna njia ambayo wakishaijua tu, matatizo yote kwa heri

Huwa nawaambia watu wazi na hapa nakuambia pia hakuna njia ya aina hiyo. Hakuna kidonge ambacho ukimeza tu matatizo yako yote yanakimbia. Zoezi la kubadili na kuboresha maisha yako ni zoezi ambalo linahitaji muda, linahitaji jitihada na linahitaji uvumilivu. Sio kitu ambachoi unafanya mara moja halafu mambo mengine yote yanakuwa shwari.

SOMA; Mambo Matano Ya Muhimu Kuyafahamu Kabla Ya Kuwekeza Kwenye Kilimo.

Hebu fikiria umeishi miaka yako yote bila ya kuwa na mipango, bila ya kuweka juhudi na kutaka kuwa tofauti. Tuseme labda umeishi hivi kwa miaka ishirini au thelathini iliyopita, halafu leo, baada ya siku moja ya ushauri maisha yako yanyooke mara moja, kwa kweli hakuna muujiza wa aina hiyo.

Kwa mfano umefanya kazi au biashara kwa miaka zaidi ya kumi na kwa miaka yote hii umekuwa hujali kuhusu kipato chako cha baadae, umekuwa huweki akiba na kipato chako hakitoshelezi hivyo unaingia kwenye madeni. Kwa miaka yote hiyo umetengeneza madeni makubwa sana na ambayo yanafanya maisha yako kuwa magumu. Halafu unataka baada ya ushauri tatizo hili litoweke mara moja, nikuambie ukweli kwamba hiko kitu hakiwezi kutokea.

SOMA; UKURASA WA 85; Jipe Miadi.

 

Kama ushauri hautakuletea majibu ya haraka, ni nini basi kitafanya hivyo?

Jibu ni hakuna. Ndio unaweza kubadili maisha yako, ndio unaweza kuondokana na changamoto na matatizo uliyonayo sasa. Ndio maisha yako yanaweza kuwa bora kuliko yalivyo sasa, ila haya yote hayatokei haraka kama mvua. Yanahitaji muda, yanahitaji wewe uone kwmaba upo kwenye tatizo na tatizo hilo halijaletwa na mtu bali wewe mwenyewe. Na pia yanahitaji uwe tayari kubadilika taratibu taratibu mpaka pale maisha yako yatakapokuwa kama unavyotaka yawe.

Katika safari hii ya mabadiliko, unaweza kuweka juhudi sana na bado usione mabadiliko, hasa mwanzoni. Hili lisikukatishe tamaa, endelea kuweka juhudi, jua kwamba kadiri siku zinavyozidi kwenda unazidi kuwa imara, unazidi kuwa bora.

SOMA; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea 

 

Nakuomba na kukusihi sana uondokana na dhana hii kwmaba mabadiliko ya maisha yako yatatokea haraka sana. Jua kabisa hili nizoezi ambalo linahitaji muda najuhudi za makusudi. Kama umetumia miaka 10 kuharibu maisha yako, mwaka mmoja pekee hautoshi kuyarekebisha. Hivyo jipe zaidi ya mwaka mmoja ili kuweza kufikia kile ambacho unahitaji kwenye maisha yako.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kubadili maisha yako. Karibu tuonane, tuzungumze na jambo ambalo unaliona gumu wewe mwenyewe utaanza kuliona ni la kawaida tunapolijadili kwa kina. Kwa ajili ya kuonana kwa ushauri piga namba 0717396253.

TUPO PAMOJA.

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu. Kama unahitaji ushauri wa haraka wasiliana na mimi kwa email makirita@kisimachamaarifa.co.tz au simu 0717396253/0755953887.

Kabla ya kutoa changamoto yako pitia changamoto ambazo tayari zimejadiliwa ili usirudie ambayo imeshajadiliwa. Bonyeza hapa kusoma changamoto zilizojadiliwa.

kitabu-kava-tangazo4322

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: