Ni kauli maarufu sana kwenye biashara kwmaba MTEJA NI MFALME. Kauli hii ni kweli ila sio kweli mara zote na kwa hali zote. Kuna wakati ambapo mteja anaacha kuwa mfalme. Ni muhimu kujua wakati huo ili usiendelee kupoteza muda mwingi kwa mteja ambaye sio sahihi kwako.
Mteja ni mfalme kwa maana kwamba anatakiwa kupewa kipaumbele cha kwanza kabisa. Kwa sababu lengo kubwa la biashara ni kutengeneza mteja, kama hujali wateja na kuwapa kipaumbele basi utawapoteza.
SOMA; Wajasiriamali Wenye Mafanikio Hufanya Mambo Haya Matano Kila Siku.
Lakini pia wateja wote hawafanani. Kuna wateja ambao unaweza kufanya nao biashara vizuri na wote mkaridhika na kuna wateja ambao unafanya biashara nao halafu wote mnatoka na hasira.
Ni wakati muhimu kwako kuanz akuwamulika wateja wako ili kujua ni wapi ambao ni wafalme kweli na wapi ambao hawafai kuwa wafalme kwako.
Leo katika mbinu hizi za kuboresha biashara yako nakushirikisha sehemu ambazo mteja anaacha kuwa mfalme;
1. Pale mteja anapofikiri anaijua biashara unayoifanya kuliko wewe. Hapa chukua hatua mara moja maana ufalme huu hautakuletea mazingira mazuri.
2. Pale mteja anapojali maslahi yake yeye tu na kufanya nae biashara kuna athiri biashara yako kwa kiasi kikubwa.
3. Pale mteja anapokuwa mtu wa madeni sugu au wa kusisitiza kupunguziwa bei hata kama itakuletea hasara.
Katika hali hizi, kuendekeza ufalme wa mteja kutaidhuru biashara yako kama vile nchi yenye mfalme mbovu inavyoangamia.
SOMA; Mambo Matano Ya Muhimu Kuyafahamu Kabla Ya Kuwekeza Kwenye Kilimo.
Wajue wateja wako vizuri na ujue wapi ni wafalme kweli na wapi ambao hawastahili kupewa ufalme.
Je ambao sio wafalme unawachukulia hatua gani? Utajifunza hili kwenye mbinu ya kesho. Usikose kusoma hapa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa ushauri wa biashara piga simu 0717396273.